LIVE STREAM ADS

Header Ads

ASHA HUSSEIN WA KIRUMBA MWANZA AFUNGA NDOA ABDULRAHMAN MAPANDE WA JIJINI DAR ES SALAAM.

Kushoto ni Bwana harusi Abdulrahman Ally Mapande Mkazi wa Dar es salaam akiwa na Bibi harusi Asha Hussein (Katikati) mkazi wa Kirumba Ilemela Mkoani Mwanza baada ya kufunga ndoa iliyofanyika March 27 Kirumba Mkoani Mwanza. Kulia ni Mama Mdogo wa bibi harusi aitwae Hawa Khalid.
Picha na Abdilah Mbaraka
Bwana harusi Abdulrahman Ally Mapande (Kushoto) Mkazi wa Dar es salaam akiwa na Bibi harusi Asha Hussein (Kulia) mkazi wa Kirumba Ilemela Mkoani Mwanza baada ya kufunga ndoa iliyofanyika March 27 Kirumba Mkoani Mwanza wakipata msosi.
Nyakati nyeti za Msosi zikiendelea katika Ukumbi wa PK Hotel Jijini Mwanza...Ahsante Ujiji Catering iliyopo Kirumba kwa msosi wa maana. Mawasiliano 0713/ 0767 50 98 98
Bwana harusi akiweka Sahihi katika hati ya ndoa.
Kutoka Kushoto ni Maalimu Sululu Salum imamu wa Msikiti wa Shamsia Kirumba akifungisha ndoa. Anaefuata ni Sheikh Omary Chamtungi akifuatiwa na Mjomba mkubwa wa bibi harusi aitwae Idrisa Ramadhan Hayesh na wa mwisho ni Mjomba wa bibi harusi Katumba Khalid Madua a.k.a Mc Katumba.
Wanafamilia upande wa bibi harusi wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi. Kutosha kushoto waliokaa ni bibi mdogo wa bibi harusi aitwae Zainabu Ibrahim, akifuatiwa na bibi mzaa bibi harusi aitwae Binti Issa Selman Katumba na wa mwisho kulia ni mama mzazi wa bibi harusi aitwa Khadija Khalid Madua.
Bibi harusi Asha Hussein (wa tatu kutoka pande zote) akiwa na mmewe akitoka nyumba kwao kwenda kwa mmewe baada ya kufunga ndoa. Wengine ni wanafamilia upande wa mme.
Wajomba wa bibi harusi wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi.
Wanafamilia upande wa bibi harusi wakiwa katika picha ya pamoja na bibi harusi.
Kushoto ni Mc Katumba ambae alikuwa ni mjomba mtu (bibi harusi) akiwa na Mc.Magoma ambae alikuwa Mc wa shughuli hiyo.
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTION 0757 43 26 94
Kwa shughuli U0MC wasiliana na Mc Katumba kwa nambari 0767 50 98 98

No comments:

Powered by Blogger.