BINAGI TV: FURSA YA MHADHARA NA MAFUNZO YA UFUGAJI WA SAMAKI.
Na:George GB Pazzo
Wananchi
na Wakazi wote wa Kanda ya Ziwa wamehamasishwa kuhudhuria Mafunzo ya Ufugaji wa
Samaki Kibiashara yanayotarajiwa kufanyika Wiki hii katika Ukumbi wa Midland
Hotel Jijini Mwanza.
Wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na
Mifugo, JKT Buramba Bunda, Japani pamoja na Ujerumani wanatarajiwa kuwepo kwa
ajili ya kutoa elimu ya mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Kampuni
inayowawezesha wajasiriamali mbalimbali hapa nchini ya PSP Mwezeshaji
Concultancy.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika Kesho kutwa Alhamisi ya April
16 Midland Hotel kuanzia saa 06:00 za Jioni hadi saa 08:00 za Usiku kwa gharama
ya Shilingi 65,000 ikiwa ni gharama ya mafunzo pamoja na chakula cha usiku.
Mkurugenzi wa PSP Mwezeshaji Concultancy Protase
Semuhomyi amewasihi wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya Mafunzo ya Ufugaji wa
Samaki Kibiashara kwa lengo la Kujikomboa kiuchumi hususani katika kipindi hiki
ambacho Taifa linakabiliwa na uhaba wa ajira.
Ili
kuthibitisha Ushiriki wako katika Mafunzo hayo, wasiliana na Waandaaji wake kwa
nambari +255 784 690 712, +255 753 778 571, au +255 766 09 41 10.
CREDIT:PSP MWEZESHAJI CONSULTANCY
No comments: