LIVE STREAM ADS

Header Ads

KARIBU KATIKA MATANGAZO YETU YA BINAGI RADIO MOJA KWA MOJA KUTOKA MAGU MKOANI MWANZA.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akishiriki katika Ujenzi wa Choo cha Shule ya Msingi Moha Wilayani Magu alipotembelea Ujenzi wa Majengo Mapya ya Shule hiyo Wiki iliyopita ambapo kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza aliahidi kutoa Mifuko 20 ya Simenti kwa ajili ya kusaidia katika Ujenzi wa Shule hiyo.
Na:George GB Pazzo
Ujenzi wa Shule ya Msingi Moha iliyopo Kata ya Magu Mjini Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza unatarajiwa kukamilika hivi karibuni, ambapo wadau mbalimbali wa Elimu wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchangia ujenzi huo ili kukamilisha Ujenzi wa Madarasa pamoja na Vyoo katika Shule hiyo.

Shule hiyo ambayo ilianzishwa tangu mwaka 2006 baada ya kugawanywa kutoka Shule ya Msingi Isandura Wilayani humo, awali ilikuwa ikitumia madarasa ya Shule ya Msingi Isandura huku jitihada za kutafuta eneo la ujenzi wa majengo yake zikiendelea.

Hata hivyo wanafunzi wa Shule hiyo walijikuta katika changamoto ya kupata elimu baada ya yao kufungwa tangu February 23 mwaka 2013 kutokana na vyumba vya madarasa walivyokuwa wakivitumia kuchakaa na hivyo kuonekana kuhatarisha maisha yao pamoja na walimu wao pia.

Kutokana na hatua hiyo, wanafunzi wa Shule hiyo walihamishiwa katika Shule za Msingi za Itumbili, Nyalikungu, Magu, Isandura na Nyambitilwa zote kutoka Wilayani Magu jambo ambalo lilisababisha msongamano mkubwa wa wanafunzi katika shule hizo.

Hatimae Ujenzi wa Shule hiyo ya Moha ulianza mwaka 2011 katika kitongoji cha Isandura B Kata ya Magu Mjini Wilayani Magu ambapo wananchi waliweza kushiriki katika ujenzi wa Shule hiyo kwa kila Kaya kuchangia Shilingi Elfu nane Mia Tano na hivyo kiasi cha shilingi Milioni tatu, laki sita na elfu hamsini na mia tano kupatikana huku Halmashauri ya Wilaya ya Magu ikichangia shilingi Milioni ishirini na mbili pamoja na Mfuko wa Jimbo (Magu) ukichangia Mifuko 200.

Michango hiyo ilifanikisha ujenzi wa Majengo matatu ya madarasa katika shule hiyo ambayo yapo katika hatua ya umaliziaji pamoja na ununuzi wa dawati 23 ambapo ujenzi wa  vyoo vyenye matundu kumi na sita unaendele kwa ushirikiano wa nguvu za wananchi pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Magu.

Hayo yalielezwa wiki iliyopita katika Risala ya Ujenzi wa Shule hiyo ya Msingi Moha, wakati Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu alipotembelea shule hiyo ili kujionea ujenzi wake unavyoendelea.

Akizungumza baada ya kujionea Ujenzi wa Shule hiyo, Mtaturu kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza aliahidi kuchangia Mifuko Ishirini ya Simenti kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Vyoo shuleni hapo ambapo alitoa rai kwa diwani wa Kata ya Magu Mjini Mussa Paul Mabelele kwa Kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Magu kushirikiana na wananchi ili kuhakikisha kuwa Ujenzi wa Vyoo pamoja na madara ya ya Shule hiyo unakamilika mapema ili wanafunzi wapate fursa ya kupata elimu.

Mtaturu ambae alikuwa Wilayani Magu kwa ziara ya Siku mbili pamoja na shughuli nyingine, pia alipata fursa ya kuwahutubia wananchi Wilayani humo katika Mkutano wa hadhara ambao ulifanyika katika Uwanja wa Sabasaba ambapo alibainisha kuwa tatizo la maji Wilayani Magu linaendelea kutafutiwa ufumbuzi huku akibainisha kuwa tatizo hilo linasababishwa na Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Ukandarasi ya KOI kushindwa kumaliza kazi yake ya upembuzi kwa ajili ya Mradi Mkubwa wa  Maji Wilayani humo.

Alisema kuwa kwa takribani Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza alizofanya ziara alikutana na tatizo la Mkandarasi huyo kuchelesha ukamilishaji wa Miraji ya Maji jambo ambalo alisema kuwa atamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Jakaya Kikwete kupitia watendaji wake asipate kazi tena katika nchi hii.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye kofia) pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali Wilayani Magu akishiriki katika Ujenzi wa Choo cha Shule ya Msingi Moha Wilayani Magu alipotembelea Ujenzi wa Majengo Mapya ya Shule hiyo Wiki iliyopita ambapo kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza aliahidi kutoa Mifuko 20 ya Simenti kwa ajili ya kusaidia katika Ujenzi wa Shule hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kulia) akizungumza na wananchi wa Magu katika Mkutano wa hadhara uliofanyika wiki iliyopita katika Uwanja wa Sabasaba Wilayani Magu ambapo kushoto ni Mhandisi Joseph Bundala ambae ni Meneja Mamlaka ya Maji Wilayani Magu akitoa ufafanuzi wa lini tatizo la Maji litaisha Wilayani Magu ambapo aliahidi kuwa tatizo hilo linashughulikiwa na muda si mrefu litakuwa limetatuliwa.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA HABARI KWA NJIA YA SAUTI.

CHANZO: RADIO METRO FM

No comments:

Powered by Blogger.