LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMATI YA SIASA YA CCM WILAYA YA NYAMAGANA MKOANI MWANZA YAKUTANA KUWEKA MAMBO SAWA.

Ikiwa imesalia siku moja Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu afanye ziara katika Wilaya ya Nyamagana, jana alikukutana na Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya hiyo katika kikao cha ndani kilichofanyikia katika Ukumbi wa CCM Wilaya ya Nyamagana kwa ajili ya Kuzungumzia masuala mbalimbali ya Kiutendaji. Baada ya kikao hiki kilifuata kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Nyamagana.

Ziara hiyo inatarajia kufanyika Kesho Jumamosi April 25 ambapo atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ili kujionea namna utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ilivyotekelezwa pamoja na Kuwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika eneo la Igoma Stand kuanzia saa Tisa Mchana.
Na:George GB Pazzo
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akiwa pamoja na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Nyamagana (kulia).
Viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Viongozi wa Chama Mkoa wa Mwanza
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM ambae pia ni Katibu siasa na Uenezi wa Chama hicho Mkoa wa Mwanza Simon Mangelepa.
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTIONS

No comments:

Powered by Blogger.