LIVE STREAM ADS

Header Ads

PAMBANO LA MAYWEATHER NA PACQUIAO KUAHILISHWA.

Na:Genya Richard
Huku ulimwengu ukiwa unajiandaa kushuhudia pambano la kukata na shoka kati ya mabondia wawili Manny Pacquiao na Floyd Mayweather linalotarajiwa kufanyika siku tisa zijazo imefahamika kuwa mkataba wa pambano hilo bado haujatiwa saini.

Wakati Mabondia hao wakiwa kwenye mandalizi ya mwisho ya pambano hilo kubwa la masumbwi duniani linasubiriwa na wapenzi wengi wa masumbwi na hata wale wasio na upenzi na mchezo huo, Promota wa Manny Pacquiao ambaye anaitwa Bob Arum amethibitisha kuwa mikataba ya pambano hilo bado haijatiwa saini na pande mbili zinazohusika.

Arum amesema kuwa sehemu ya mkataba ambao alipewa mwezi huu haukuwa katika makubaliano yao na upande wa Mayweather Promotion pamoja na kampuni ya MGM.
Kauli hiyo inakuja huku tayari tiketi za pambano hilo zikiwa zimeingia sokoni usiku wa kuamkia leo.

Hata hivyo taarifa hizo zimekanushwa vikali na upande wa Mayweather Promotion ambapo mkurugenzi wake Leonard Ellerbe amesema kuwa kinachomtatiza Arum ni kipengele cha mkataba ambacho kinamzuia kutokuwa na haki za kusimamia kila kitu kuhusu pambano hilo.

Mkurugenzi huyo waMayweather amekwenda mbali zaidi na kumtuhumu Bob Arum kwa kusema kuwa amekuwa akipanga njama na mawakili wake za kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba wapambano hilo na amehtibitisha kuwa kila kitu kuhusu pambano hilo kinaendelea kama ilivyopangwa.

Manny Pacquiao na Floyd Mayweather waanatarajiwa kupanda ulingoni Mei mbili katika pambano linalosubiriwa kwa hamu kubwa huku kila upande ukiwa unajigamba kushinda pambano hilo.

Moja kati ya vitu vinavyoongeza ladha ya pambano hilo ni rekodi ya kutopigwa ya Floyd Mayweather ambaye wengi waanamini kuwa ana nafasi kubwa ya kupoteza mchezo huo kutokana na ubora wa Manny Pacquiao.

Mshindi katika Pambano hilo atajinyakulia kitita cha fedha takribani Bilioni 160 za kibongo baada ya kukatwa kodi ya takribani asilimia 30.

Tusubiri siku hiyo mpenzi msoma wa Binagi Media Group ili tuone itakuwaje.

No comments:

Powered by Blogger.