LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU WA CCM MKOA WA MWANZA MIRAJI MTATURU KUTIKISA WILAYA ZA NYAMAGANA NA ILEMELA.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangelepa akitoa taarifa ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza kwa Wanahabari katika Ofisi za Chama hicho Mkoa.
Na:George GB Pazzo
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu anatarajia kufanya ziara katika Wilaya za Nyamagana na Ilemela, ikiwa ni katika Kuhitimisha ziara yake katika Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza ambayo aliianza Mwishoni mwa Mwezi uliopita Wilayani Ukerewe.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama hicho Mkoa wa Mwanza Simon Mangelepa, ameeleza kuwa Mtaturu ataanza kwa kufanya ziara katika Wilaya ya Nyamagana kesho kutwa Jumamosi April 25 ambapo anatarajia kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo kabla ya kuwahutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika eneo la Stand ya daladala ya Igoma.

Mangelepa amefafanua kwamba baada ya ziara hiyo, Mtaturu atahitimisha ziara hiyo Jumatatu ijayo ya April 28 katika Wilaya ya Ilemela ambapo pia anatarajia kutembelea na kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Wilaya hiyo ambapo pia atawahutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Magomeni Kata ya Kirumba.

Wananchi wote wametakiwa kuhudhuria katika Mikutano yote ya hadhara itakayofanyika katika Wilaya zote mbili za Nyamagana na Ilemela, bila kujali itikadi zao za Kisiasa kwa Kuwa masuala mbalimbali ya kimaendeleo yanayowahusu yatazungumzwa katika Mikutano hiyo ambayo itakuwa ikianza majira ya saa tisa Mchana.

Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu ilianza March 22 mwaka huu katika Wilaya ya Ukerewe na kufuatia katika Wilaya za Sengerema, Misungwi, Kwimba pamoja na Magu ambapo katika ziara hiyo pamoja na mambo mengine, pia Mtaturu alipata fursa ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kujionea namna Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya Mwaka 2014/15  inavyotekelezwa.
                                                                 Credit:Radio Metro

No comments:

Powered by Blogger.