LIVE STREAM ADS

Header Ads

MTATURU AKUTANA NA KAMATI YA SIASA WILAYA YA ILEMELA KABLA YA KUANZA ZIARA YAKE WILAYANI HUMO.

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilemela ikiwa katika Kikao cha ndani hii leo. Kamati hii inakutana ikiwa zimesalia siku nne kabla ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu kufanya ziara Katika Wilaya ya Ilemela ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Wilaya hiyo kwa ajili ya kujionea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/15.Baada ya Kikao hiki, pia kitafuata kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilemela.
Lakini pia atawahutubia wananchi katika Mkutano wa Hadhara utakaofanyika siku ya ziara hiyo ambayo ni Jumatatu ijayo ya April 28 kuanzia majira ya saa tisa mchana katika Uwanja wa Magomeni Kata ya Kirumba.
Na:George GB Pazzo
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akisaini kitabu cha wageni baada ya Kuwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilemela uliopo Pasiansi. Kushoto kwake ni viongozi wa Chama hicho Wilaya ya Ilemela.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilemela.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Simon Mangelepa akisaini kitabu cha wageni.
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTIONS.

No comments:

Powered by Blogger.