LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU WA CCM MKOA WA MWANZA AITAKA SERIKALI KUWALIPA WAALIMU STAHIKI ZAO.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (katikati) akizungumza jana katika Kikao cha Halmashauri kuu Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza. Kulia ni Nelson Mesha ambae ni Mwenyeki wa Chama hicho Wilaya ya Ilemela na Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya hiyo Loth Olelemeirut. 
Na:George GB Pazzo
Serikali imetakiwa kuhakikisha kuwa inawalipa Waalimu stahiki zao zote ili kuondoa Malalamiko ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakitolewa na Waalimu kutokana na kutolipwa stahiki zao kwa wakati.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu, katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Ilemela kilichofanyika katika Ukumbi wa Maliasili Pasiansi Wilayani humo.

Mtaturu alibainisha kuwa deni la waalimu hapa nchini limekuwa likiongezeka siku hadi siku kutokana na baadhi ya Watumishi wa Serikali katika ngazi za halmashauri kutumia fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya Kuwalipa Waalimu kutumika kwa ajili matumizi mengine ambayo hayakukusudiwa.

Alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikipelekea hasira na malalamiko makubwa kutoka kwa waalimu jambo linalopekea Chama Cha Mapinduzi CCM kulaumiwa kwa kuwa ndicho chama kilichoko madarakani.

Mtaturu aliiomba Serikali kufuatilia fedha zinazotengwa kwa ajili ya kuwalipa waalimu ili kujihakikishia kama fedha hizo zinawafikia Waalimu jambo ambalo amesema kuwa litasaidia kuondoa kero na malalamiko ya waalimu yanayotokana na deni wanaloidai serikali.

Aidha aliwasihi watumishi wa Serikali kuzingatia Utumishi bora kwa waalimu ikiwa ni pamoja na kuhakikishakuwa  hakuna mwalimu anaeidai Serikali wala mwalimu ambae hajapandishwa cheo baada ya kuhitimu masomo yake.

Katika hatua nyingine aliwasihi watumishi hao kutowahamisha waalimu kutoka katika vituo vyao vya Kazi kama Halmashauri zao hazina fedha za kuwalipa waalimu hao jambo ambalo amesema kuwa litasaidia kuondoa ongezeko la deni ambalo waalimu wanaidai serikali.

“Naomba niwaambiwe waalimu CCM haijawahi kuzuia fedha zenu na wala haina mpango wa kuzuia fedha hizo ambapo tunaendelea kusema Serikali ihakikishe kuwa inawalipa waalimu fedha zao hivyo sisi tusipewe mzigo usio wetu”.Alisisitiza Mtaturu.

Kwa mjibu wa Chama cha Waalimu nchini CWT kupitia kwa Rais wa Chama hicho Gratian Mukoba ilielezwa kuwa hadi mwishoni mwa mwaka jana Serikali ilikuwa ikidaiwa na Waalimu zaidi ya Shilingi Bilioni Kumi.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (katikati) jana akiwa katika Kikao cha Halmashauri kuu Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza. Kulia ni Nelson Mesha ambae ni Mwenyeki wa Chama hicho Wilaya ya Ilemela na Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya hiyo Loth Olelemeirut. 
Viongozi wa CCM na Serikali Mkoani Mwanza.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilemela.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilemela.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Manju Msambya.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilemela Nelson Mesha (katikati) akizungumza katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilemela.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Loth Olelemeirut (katikati) akizungumza katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilemela.
CREDIT: RADIO METRO

No comments:

Powered by Blogger.