LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII. NI BAADA YA KULALAMIKIA GHARAMA ZA MATIBABU.

Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (mwenye miwani) ikiwa katika Hospital ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure juzi Jumamosi baada ya Katibu huyo kufanya ziara ya Kushtukiza katika Hospitali hiyo ili kujionea hali ya utoaji wake wa huduma kwa wananchi ambapo alibaini uwepo mkubwa wa idadi ya wagonjwa wanaoitegemea hospitali hiyo kiasi kinachofanya dawa zinazotolewa na serikali kupitia Bohari ya dawa nchini kuisha kabla ya wakati uliokusudiwa hali inayopelekea makundi yanayopata huduma za afya bure, mfano watoto walio na umri chini ya miaka mitano kutozwa malipo hospitalini hapo.
Na:George GB Pazzo
Wananchi Mkoani Mwanza wameshauriwa Kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa lengo la kunufaika na huduma za Matibabu kwa gharama nafuu kupitia huduma ya Bima ya Afya.

Ushauri huo ulitolewa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwa katika Hospital ya Mkoa Mwanza Sekour Toure alipokuwa katika ziara ya kutembelea miradi ya  maendeleo katika Wilaya ya Nyamagana.

Mtaturu alibainisha kuwa huduma za matibabu kwa wananchi waliojiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii hapa nchini ni bora na nafuu zaidi, ambapo familia yenye wazazi wawili na watoto wanne hutibiwa mwaka mzima kwa kuchangia gharama ya shilingi Elfu Kumi.

Kauli ya Mtaturu ilijili baada ya Kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wazazi ambao waliulalamikia Ungozi wa Hospitali ya Sekour Tore kutokana na kuwauzia dawa watoto walio chini ya Umri wa Miaka Mitano huku Serikali ikiwa imetangaza kuwa matibabu kwa watoto hao ni bure.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekour Toure Dr.Brian Mawala alibainisha kuwa dawa zinatotolewa na Serikali kupitia Bohari ya dawa nchini MSD, zimekuwa hazitoshelezi mahitaji kulingana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaopokelewa Hospitalini hapo, jambo ambalo hupelekea wananchi kuhimizwa kuchangia huduma za matibabu zikiwemo huduma ambazo zinapaswa kutolewa bure ambazo ni pamoja na huduma za matibabu kwa watoto walio chini ya Umri wa Miaka Mitano.

Nae Daniel Temba ambae ni Katibu wa Afya katika Hospitali ya Sekour Toure alitoa rai kwa wananchi wanaofika katika hospitali hiyo kwa ajili ya Matibabu kutoa taarifa katika Uongozi wa Hospitali hiyo pindi wanapokutana na changamoto za aina yoyote zinazokwamisha upatikanaji wa huduma za afya hospitalini hapo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akisalimiana na Dr.Brian Mawala (Kulia) ambae ni Kaimu Mganga Mfawishi wa Hospital ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure.Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanza Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu).
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akisaini kitabu cha wageni baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu).
Daniel Temba ambae ni Katibu wa Afya katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (mwenye miwani) akiwa katika wodi ya wazazi katika Hospital ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akitoa pongezi zake kwa akina mama waliojifungua jumamosi alipotembelea hospitalini hapo.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza pia ilitembelea jengo hili ambalo linamilikiwa na CCM Kata ya Nyamagana baada ya kukamilika kwa ukarabati wake. Jengo hili linapatikana Mtaa wa Uhuru Darajani Jijini Mwanza.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza ikikagua ujenzi wa barabara ya Mawe ya Igogo Jijini Mwanza juzi Jumamosi.
Ukaguzi katika barabara ya mawe ya Igogo ambao unagharimu zaidi ya shilingi Milioni 250
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Katikati) akizungumza baada ya Kufanya ziara ya Kutembelea Ujenzi wa Maabara za Sayansi katika Shule ya Sekondari Nyabulogoya iliyopo Kata ya Butimba (Zamani) kwa sasa Kata ya Nyegezi.
Mkuu wa Shule ya Sekondary Nyabulogoya Mwl.Christine Lwamba akisoma taarifa ya Ujenzi wa Maabara katika Shule hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza (Kushoto) kwa niaba ya Chama akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Nyabulogoya (Kulia) Kiasi cha shilingi laki tatu kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Maabara katika shule hiyo.
Kutoka Kulia ni Diwani wa Kata ya Butimba (CCM) Dismas Masunu akizungumza wakati wa ziara ya Katibu wa CCM katika shule ya Sekondari Nyabulogoya iliyokuwa na lengo la kujionea ujenzi wa Maabara katika shule hiyo. Katikati ni Elias Mpanda ambae ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana na Kushoto ni Simon Mangelepa ambae ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza.
Credit:Radio Metro

No comments:

Powered by Blogger.