PLUIJM ATANGAZAKIKOSI CHA MAUAJI YA ETOILE DU SAHILE YA TUNISIA.
Picha Kutoka Maktaba
Na:Genya Richard
Kocha Timu ya Yanga
Mhoholanzi Hans der Pluijm ametangaza kikosi kitakachowavaa Watunisia hii leo
jumamosi May 2 mwaka 2015 katika Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika ambapo timu hiyo inachuana na
Etoile Du Sahile.
Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa kuanzia majira ya saa
01:00 jioni kwa saa za Afrika ya Kaskazin huku kwa saa za Afrika Mashariki
ikiwa ni saa 3.00 za jioni ambapo mechi hiyo inatarajiwa na kituo cha Azam 2
cha hapa nchini.
Timu ya Yanga Hans der PLUIJM amewataja wachezaji
watakakipiga katika mechi hiyo kuwa ni;
1.Ally
Mustapha
2.Mbuyu
Twite
3.Osca
Joshua
4.Kelvin
Yondani
5.Nadir
Haroub
6.Said
Makapu
7.Saimon Msuva
8.Salum Telela
9.Hamisi Tambwe
10..Mrisho Ngassa
11.Pah Sherman
Hicho ndicho kikosi cha kwanza cha Yanga kinachotarajiwa kupambana
na Etoile du Sahel ambapo itakumbukwa kuwa katika Mechi ya Kwanza hapa nchini timu hizo zilitoka suluhu ya 1-1, matokeo ambayo yanailazimu yanga kusaka ushindi ugenini na si vinginevyo ili iweze kusonga mbele katika michuano hiyo ya Klabu bingwa barani Afrika.
Je una maoni
yoyote kuhusu kikosi hicho? unafikri kuna sehemu ya kufanyia marekebisho ili
Yanga ifanikiwe kupata ushindi? Toa maoni yako kupitia 0713208878
No comments: