LIVE STREAM ADS

Header Ads

JIONEE ILIVYOKUWA KATIKA MAADHIMISHO YA MEI MOSI KITAIFA MKOANI MWANZA YAFANA.

Leo Tanzania imeungana na Mataifa mengine duniani kuadhimisha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyanyakazi Duniani Maarufu kwa jina la Mei Mosi ambayo Kitaifa hapa nchini yamefanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba Ilelema Mkoani Mwanza. Maadhimisho hayo yamekuwa na Mvuto wa pekee kutokana na ambavyo wananchi na wafanyakazi kutoka Sekta mbalimbali za Serikali na binafsi walivyojitokeza kushiriki na kujionea maadhimisho hayo katika Uwanja wa CCM Kirumba. 
Mgeni Rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ambapo Kauli mbiu mwaka huu katika Maadhimisho hayo ilikuwa ni "Mfanyakazi Jiandikishe, Kura Yako Ina Thamani katika Maendeleo Yetu"
Katika Picha Juu ni Maandamano ya Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza yakitoka katika Uwanja wa Furahisha yalipokuwa Mabanda ya Maonyesho ya Siku hii ya Mei Mosi yakielekea katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo katika ujumbe wa Muungano huo ulikuwa ni Kuwezeshwa Mitaji kwa ajili ya kuinua shughuli zao za Biashara, Kuendelea kutengewa Maeneo kwa ajili ya shughuli zao.
Na:George GB Pazzo
Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza.
Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza.
Maandamano ya Wafanyakazi mbalimbali yakielekea katika Uwanja wa CCM Kirumba
Wafanyakazi wa Bank ya Posta wakiingia katika Uwanja wa CCM kirumba
Wanachama wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza wakiingia katika Uwanja wa CCM Kirumba
Altaf Mansoor ambae ni Mlezi wa Timu ya Watoto wa Mitaani Mkoani Mwanza ambayo ilichukua Kombe la Dunia kwa Watoto wanaoishi Mitaa Mwana jana akiingia katika Uwanja wa CCM Kirumba hii leo huku akiwa ameshikilia Kombe la Timu hiyo.
Altaf Mansoor kutoka Kampuni ya Mafuta ya MOIL ambae ni Mlezi wa Timu ya Watoto wa Mitaani Mkoani Mwanza ambayo ilichukua Kombe la Dunia kwa Watoto wanaoishi Mitaa Mwana jana akiingia katika Uwanja wa CCM Kirumba hii leo huku akiwa ameshikilia Kombe la Timu hiyo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL wakiingia katika Uwanja wa CCM Kirumba
Taswira ya Uwanja ilivyokuwa
StarTimes Tanzania pia walikuwepo katika Maadhimisho hayo.
Viongozi wa Muungano wa Machinga wakiwa katika Studio za Radio Metro Jijini Mwanza wakielezea ushiriki wao katika Maadhimisho ya MEI MOSI.

No comments:

Powered by Blogger.