LIVE STREAM ADS

Header Ads

MASHINE ZA BVR ZAWAHESHIMU WANANCHI WA KATA YA NYAMANORO MKOANI MWANZA.

Wananchi wa Mtaa wa Mkuu Kata ya Namanoro Wilayani Ilemela jana wakiwa katika Mstari tayari kwa ajili ya Kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga Kura.
Na:George GB Pazzo
Pamoja na zoezi la Uandikishaji hapo awali kulalamikiwa kuwa limeanza kwa kusuasua katika maeneo mbalimbali hapa nchini, baadhi ya Wananchi  katika Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza wameelezea kuwa zoezi hilo limeanza vyema katika Kata hiyo.

Huku wakisema kuwa Mashine za Biometric Voter Registration BVR zimewaheshimu, baadhi ya wananchi wa Kata hiyo jana walibainisha kwamba japokuwa bado kuna idadi chache ya Mashine hizo, lakini zoezi la uandikishaji Katani hapo lilianza vyema bila kusuasua kama ilivyokuwa ikiripotiwa katika maeneo mengine.

Pamoja Daniel Dwisha pamoja na James Ntare ambao ni viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Mkudi katika Kata hiyo ya Nyamanoro walibainisha kuwa zoezi la uandikishaji ambalo lilianza jana Katani hapo lilianza Vizuri katika Vituo mbalimbali vya Kata hiyo kwani hakukua na kusuasua kwa utendaji wa Mashine za BVR.


Aidha walizidi kusisitiza kuwa ni vyema Serikali ikaongeza Mashine za BVR kwa lengo la kuongeza ufanisi katika zoezi hilo la Uandikishaji wa Wananchi katika daftari la kudumu la Wapiga Kura kwa kuwa vituo vingi katika Kata hiyo pamoja na Kata nyinginezo vina Mashine Moja jambo ambalo haliwezi kukidhi mahitaji yaliyopo.

Kama ilivyo katika Kata nyingine za Wilaya za Mkoa wa Mwanza, Kata za Nyamhongoro, Nyamanoro, Pasiansi, Kawekamo pamoja na Nyakato katika Wilaya ya Ilemela zilianza zoezi la Uandikishaji ambalo litadumu kwa siku saba kabla ya kuhamia katika Kata nyingine.
"GB PAZZO TAYARI AMEJIANDIKISHA...JE WEWE? HAKIKISHA UNAJIANDIKISHA MSOMAJI WA BINAGI MEDIA GROUP".

No comments:

Powered by Blogger.