LIVE STREAM ADS

Header Ads

BANK YA NMB YAZIPIGA MSASA SHULE NNE ZA MSINGI WILAYANI BUSEGA, SIMIYU.

Na:Prisca Mshumbuzi
Benki ya NMB imekabidhi jumla ya madawati 240 yenye thamani ya Shilingi Milioni 20 katika shule nne za Wilayani Busega mkoani Simiyu. 

Akikabidhi madawati hayo katika shule za msingi Nyanshimo jana, Mkurugenzi wa Fedha wa Benki hiyo, Waziri Barnaba alieleza kuwa benki hiyo inatoa kipaumbele katika elimu ili kuleta mabadiliko.

“Tunaelewa changamoto kubwa iliyopo katika elimu ikiwapo ya ukosefu wa madawati na ndio maana Benki ya NMB imeamua kutoa madawati katika baadhi ya shule zenye uhaba wa madawati,” alisema Barnaba.

Aidha Barnaba alisema kuwa Benki hiyo hutenga fungu kila mwaka kwa lengo la kutoa misaada kwa jamii huku akiwataka walimu na wanafunzi kuyatunza madawati hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paulo Mzindakaya, alitoa shukrani kwa Benki hiyo huku akisema kuwa imepunguza changamoto kubwa iliyokuwa ikiikabili wilaya hiyo.

“Hii Wilaya tulikuwa na changamoto kubwa maana tulikuwa na ukosefu wa madawati zaidi ya elfu moja lakini kwa haya tuliyoyapata yatatusogeza na sisi tutayatunza vizuri.” alisema Mzindakaya.

Katika Wilaya ya Busega shule zilizofanikiwa kupata msaada wa madawati hayo ni pamoja na Nyanshimo(60), Nasa(60), Sukuma(60) na Simakitongo(60).

No comments:

Powered by Blogger.