LIVE STREAM ADS

Header Ads

SEHEMU YA TANO: JIFANYIE UCHUNGUZI KATIKA MAMBO YAFUATAYO MAISHANI MWAKO.

HUMPHREY MAKUNDI (KULIA) NA
ALLARD MINJA (KUSHOTO), WOTE WANATOKA LIFE SECRETS COMPANY MWANZA.

UNA TASWIRA GANI KWENYE AKILI YAKO.
Ni mbinu au namna ya kutengeneza picha, michoro au uhuishaji ili kuweza kuwasilisha ujumbe au kupata kitu fulani.

Kila kitu ambacho unakiona hapa duniani kilianza picha fulani katika akili ya mtu na ndipo mtu huyo akaanza kukitendea kazi. Magari unayoona, nyumba na maghorofaa, ndege,michoro mbalimbali,tv, radio,simu, nguo,sufuria,vijiko yaani kila kitu unachokiona hapa duniani. Muulize Masuud Kipanya kama huwa haoni na kuichora katuni ya kipanya kila siku kwenye akili yake kabla hata ya kuiweka kwenye gazeti ili kufikisha ujumbe wa siku husika.

Kuna siku niliandika kwamba binadamu anafikiri kwa picha na kama hakuna picha mtu hawezi kufikiri vizuri au kuelewa suala fulani kwa undani, nikisema simba, mbwa, sungura, friji, gari, ndege, kuku, kunguru, tembo,raisi wa awamu ya tatu Tanzania, kitanda, kabati na vinginevyo kinachokuja kwenye kioo cha akili yako ni picha ya hivi vitu maana tunafikiri kwa picha.

Kuna mchoraji mmoja aliwahi kuulizwa nini kinafanya picha anazochora kuwa nzuri sana, nae akajibu kwamba I dream my painting then i draw it, yaani Naota mchoro wangu alafu nauchora. Nataka nikuambie kwamba hakikisha una picha halisi ya kitu unachokitaka kwanza ndipo ukaanze kufanya jitihada zote za kukitafuta. 

Kama ni biashara fulani unataka kuanza kuifanya jione kwanza jinsi unavyoifanya namna unavyohudumia wateja na jinsi wateja wanavyokuja hata kabla haujaanza kuifanya ile biashara husika, kama ni gari unataka kumiliki ona aina yake, rangi jione namna unaliendesha tayari n.k,Lakini pia kama ni nyumba ona kabisa jinsi itakavyokuwa mpaka mpangilio wake ndani wa kila kitu.

Kwa nini nimesema hivyo? Hii itakusaidia wewe kupata kitu ambacho moyo wako ulikitaka kwa 100%, Lakini pia itakusaidia kutokukata tamaa wakati unakifuatilia maana tayari una picha halisi maadamu umeshaacha alama kwenye sehemu ya akili yako inayoitwa akili iliyolala (sub councious mind) na tafadhali usisahau kwamba umiliki unaanzia kwenye akili kwanza. Leo hii muulize Mengi kama hatakwambia alimiliki vituo vya redio na Tv hata kabla nyie hamjaviona.

Nakumbuka kuna mahojiano niliwahi kusikiliza ambayo mwanamuziki maarufu duniani Celine Dion alikuwa anahojiwa akaulizwa hivi katika maisha yake aliwahi kujiona au kufikiri kwamba kuna siku atakuwa anaimba na mamilioni ya watu wakimtazama naye akajibu tangia akiwa na umri wa miaka 6 alishajiona anaimba kwenye steji na mamilioni ya watu wakimshangilia.Sasa kwa mtu ambaye haelewi namna akili iliyolala na akili ambayo haijalala zinavyofanya kazi atasema alikuwa anajisifia lakini hakuwa anajisifia ila ni kweli alishaona hiyo hali ni hiko ndicho kilikuwa kinamsukuma kuendelea kujituma na kuandika nyimbo kila siku. 

HIi inadhihirisha pia umiliki wa kitu unaanzia kwenye akili na kabla huajaanza kufanya na kutafuta kitu unachokitaka tengeneza picha halisi ya hicho kitu kwenye akili yako kwanza ndipo ukakifanye.

Unajua ubaya ni kwamba watu wazima huwa wanafikiri kwamba kwa wao kukaa chini na kutengeneza taswira fulani ya kitu wanachokitaka ni kazi ya watoto wadogo kufanya lakini sio kweli...Jaribu kuvuta picha kipindi ukiwa mtoto ulikuwa unaona kila kitu kinawezekana na unaweza ukakipata kwa hivyo mara kadhaa ulienda kwa wazazi na kutaka kitu hiki na kile, pindi ambapo wazazi walikuwa hawawezi kukupatia kitu fulani walikuacha na alama ya kujiuliza kwamba kuna vitu unaweza kupata na kuna ambavyo huwezi umekuwa na hali hii mpaka saizi kwa hiyo wamekuingizia programu yao katika akili yako ila unao uwezo wa kuiondoa na kuingiza programu yako mwenyewe maana kiuhalisia unao uwezo wa kupata chochote kile unachokitaka.

Wanasaikolojia wamedhihirisha kwamba kitu chochote ambacho akili yako (akili iliyolala)inaweza kukitengenezea taswira na ikakaa nacho kwa muda mrefu akili inao uwezo wa kukimiliki, una taswira gani katika akili yako? Unaona nini kwenye taswira yako? hicho unachokiona Nakuhakikishia kama unafuata ushauri tunaotoa kwa kifupi hapa na kuutendea kazi kila siku unao uwezo wa kukipata . 

Ole wako unaeona kushindwa,kurudi nyuma ,kuanguka,kufilisika maana utapata hicho hicho ni suala la (WYSIWYG) what you see is what you get yaani KILE UNACHOKIONA NDICHO UTAKACHOKIPATA.
Mwisho

IMEANDALIWA NA LIFE SECRETS COMPANY YA JIJINI MWANZA AMBAO NI WATAALAMU WA AFYA NA MAENDELEO BINAFSI.
Email:allnhumph@gmail.com Phone: 0689 45 26 70/0765 53 68 42
Soma HAPA Sehemu ya Nne
Powered by Blogger.