MAKALA FUPI: NJIA BORA ZA KUULINDA MTAJI WA BIASHARA YAKO.
Simu:0754 551 306
Ndugu msomaji imekuwa kawaida sana kusikia wanadamu kila kukicha wakiweka mipango ya usalama wa maisha yao, kama kuwa na afya bora, usalama wa maisha yao kwa kuwa na nyumba yenye ulinzi, gari lisilo na matatizo, lakini imekuwa vigumu sana kusikia wajasiriamali wakijadili usalama wa mitaji yao.
Hali hii imekuwa ikiwasababishia wengi wao maumivu makubwa hasa baada ya kupoteza mitaji yao, kwa kuwa tu walishindwa kuilinda kwa kujua njia bora za kulinda mitaji ya bishara zao.
Nimeona ni vyema kuleta makala hii yenye kutoa elimu ya namna ya kulinda mtaji wa bishara yako, muda mfupi uliopita niliwasilisha maudhui haya kwenye kituo cha redio cha Metro Fm klichopo Jijini Mwanza.
Lakini nikaguswa pia kuandika katika fasihi andishi ili kazi hii iweze kuishi milele na milele na kusomwa na watu wengi, ambapo naamini italeta mageuzi makubwa katika ubongo wa Wasomaji wake.
Zifuatazo ni njia bora za kulinda mtaji wa bishara yako, ungana nami katika ukurasa huu.
Njia ya kwanza; ni kutunza kumbukumbu za bishara yako, jenga desturi ya kuweka kumbukumbu za mauzo ya bishara yako kila siku, hii itakusaidia kutathimini bishara yako na hatimaye kujua mwenendo wa bishara yako.
Watu wengi weliofanikiwa kama Bill Gates, Mengi na wengineo wamekuwa na utaratibu mzuri wa kutunza kumbukumbu za bishara zao.
Njia ya pili; ni kutenganisha biashara yako na urafiki hasi, epuka kuwa na marafiki walio na ajenda ya kunufaika kupitia urafiki wako, kwani moja ya matokeo yake ni kukuingiza kwenye mitego ya kiuchumi ili na wao waweze kupata chochote.
Kuna mfano hai wa rafiki yangu mmoja alijikuta anafirisika baada ya kupata ushauri mbaya wenye manufaa kwa rafiki yake baada ya kushauriwa anunue gari la kutembelea ili wawe wanatoka Out wikiendi badala ya kujenga nyumba ya bishara na kuikuza zaidi.
Njia ya tatu; Ni wekeza faida unayoipata katika bishara ya kwanza kwenye biashara ya pili na hata ya tatu na kuendelea ili izalishe zaida maradufu na kukusaidia kuzidi kupata faida kubwa inayoweza kukusaidia kufanya kitu kingine kikubwa kwa mara moja, kama kujenga nyumba au kufungua duka.
Hapa natoa angalizo, kuna wafanyabishara wengi wanatumia faida kwa mambo yasiyo ya kimsingi kama kulewa, na mavazi ya kifahari nk. Kumbuka hayo si matumizi sahihi ya faida uipatayo katika biashara yako.
Njia ya nne; Ni kuwa mkarimu wakati wote wa kufanya bishara yako, ukarimu ni sumaku ya kuvuta wateja, hakikisha una kuwa na wafanyakazi waliofundishwa ukarimu kwenye bishara yako na matokeo yake ambayo ni biashara yako kustawi utayaona.
Njia ya tano; Jitenge wewe na bishara yako, siku zote ione bishara yako kama mtu mwingine anayehitaji kuheshimiwa, jione kama wewe ni mfanyakazi uliyepewa kazi ya kuifanya bishara hiyo ili ikue, hiyo itakusaidia kuwa na nidhamu juu ya bishara yako.
Njia ya sita; baini mbinu mpya zenye kuleta tija katika bishara yako, muda wote jikite kwenye kufanya tafiti na kubaini njia mpya zinazoweza kuongeza wateja katika bishara yako.
Mfano kuna mfanyabishara mmoja wa bucha ya kuuza nyama aliamua kutoa ofa ya kila anayenunua nyama kwake anapata nyanya mbili bure, mbinu hiyo kiukweli ilivuta wateja wengi kwake na hivyo kustawisha biashara yake.
Njia ya saba; Tafuta uzalishaji nafuu wa bishara yako, kumbuka hakuna mteja anayependa kuumia katika upande wa bei ya huduma au bidhaa fulani,ukiwa na uzalishaji wa chini wa bidhaa zako itakusaidia kuweka bei kuwa ya kawaida na wateja wengi kuimudu.
Bila shaka wewe msomaji umefuatilia kwa makini Makala hii na naamini kila jambo linawezekana kama litafunguliwa njia, na njia hiyo ni wazo litakaloiingia kwenye utekelezaji na uthubutu.
Neno la faraja ni kwamba "kuzaliwa maskini sio makosa bali kufa maskini ni makosa".
No comments: