SIKILIZA WALICHOKISEMA MADAM RITA, MASTER J NA SALAMA KUHUSU SHINDANO LA BSS 2015.
Majaji wa Shindano la Kusaka Vipaji hapa
nchini la Bongo Star Search wamesema kuwa maboresho makubwa yamefanyika katika kuliboresha
shindano hilo hivyo mwaka huu litakuwa tofauti ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmack
Production inayoandaa shindano hilo Rita Paulsen maarufu kwa jina la Madam Rita
ambae pia ni Jaji Mkuu pamoja na Majaji wasaidizi Master na Salama Jabiri
walibainisha hayo wikendi iliyopita Jijini Mwanza wakati wa Usaili wa kuwasaka
wawakilishi watakaoiwakilisha Kanda ya Mwanza katika Shindano hilo litakalofanyika
Jijini Dar es salaam.
“Mashindano ya Mwaka huu yanafanyika mwaka
wa nane hivyo uzoefu wa miaka minane ni Mkubwa sana na kama unavyoona tumeanzia
huku (Mwanza) halafu tutaenda Arusha, Mbeya na Dar es salaam…aaaah changamoto
zipo kila siku maana kitu chochote kizuri hakikosi changamoto na changamoto
zipo nyingi lakini tunazimudu”. Alisema Madam Rita ambae alibainisha kuwa BSS
2015 itaanza kuruka hewani kuanzia Julai 19 mwaka huu kupitia Star Tv na Clouds
Tv.
“Kwa ufupi BSS tunasaka Vipaji na
inshu mhimu ambayo tumeboresha mwaka huu ni malalamiko mengi ambayo tumekuwa
tukiyasikia kwamba washindi inakuwaje mbona hawasikiki kwenye soko la muziki
baada ya kushinda BSS…Ni inshu ambayo ilikuwa siyo kosa letu maana sie tulikuwa
tukijua tukimpa mtu hiyo Milioni Hamsini ataenda kuwekeza kwenye Muziki kumbe
walikuwa wanafanya vitu kinyume…Kuna warembo, gari, wapambe na pamba vilikuwa
vinawachanganya hivyo mwaka huu tumebadilisha mfumo na tumesema washindi
watakaoingia tano bora watasimamiwa na Tip Top Connection ili ile hela
tuiwekeze kidogo kwenye muziki na tupunguze hizi lawama lawama”. Alisema Master
J.
“Haya ni mashindano na sidhani kama
kuna haja ya Kumwambia mtu kitu ambacho siyo sahihi, kama anakuja na hajui
kuimba inabidi aambiwe kuwa hajui kuimba na kama anajua kuimba inabidi aambiwe
kuwa anajua kuimba…Master J ni Producer Mkubwa na ndiyo maana Rita amemchagua
kuwa hapa na mimi namshukuru masikio yangu ni mazuri hivyo kama ni kutenda haki
tunajitahidi kila siku kutenda haki na kumwambia mtu kile anachostahili ili
kama hawezi asipoteze muda wake”. Alisema Salama Jabir.
Bonyeza HAPA Kuona Picha za Usaili wa BSS 2015 Mwanza.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
No comments: