LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKURUGENZI WA MABASI YA J4 ATIWA MBARONI JIJINI MWANZA KWA TUHUMA ZA MAUAJI.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo akitoa taarifa kwa wanahabari hii leo ofisini kwake baada ya tukio la mauaji ya watu wawili Jijini Mwanza lililotolea usiku wa kuamkia leo majira ya saa nne usiku eneo la Buzuruga ambapo anaetuhumiwa kutekeleza mauaji hayo ni Mkurugenzi wa Mabasi ya J4 yanayofanya safari zake katika Mikoa ya Mwanza na Mara.
 Na:Binagi Media Group
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya J4 Juma Mahende (45) Mkazi wa Nyakato Sokoni Jijini Mwanza, kwa tuhuma za mauaji ya kuwapiga risasi Watu wawili.

Akizungumza jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi Majira ya Saa nne Usiku katika eneo la Stand ya Buzuruga Jijini Mwanza.

Alisema kuwa mauaji hayo yalitokea baada ya kuibuka mzozo baina yao ambapo mtuhumiwa huyo ambaye hatimae alitoa bastora yake na kuwafyatulia risasi na hivyo kuwauwa papo hapo watu hao ambao ni Ally Mohamed (35) Mkazi wa Igoma na Cloud Steven Mwenye (39) Mkazi wa Nyasaka.

“Wakati Mkurugenzi wa magari ya J4 yanayofanya safari zake katika Mikoa ya Mwanza na Mara anafunga ofisi yake majira yaa saa nne usiku, walitokea vijana wawili ambao walianza kuzozana nae kabla ya Mkurugenzi huyo kutoa bastora na kuwafyatulia risasi za kifuani watu hao hao na kuwaua”.

Kamishina Msaidizi Mkumbo aliitaja Silaha iliyotumika katika mauaji hayo kuwa ni bastola aina Browning yenye nambari 00092890 ambapo Polisi wanaendelea na uchunguzi wake ili kubaini chanzo cha mauaji hayo kabla ya kumfikisha kizimbani mtuhumiwa huo ili kujibu shitaka linalomkabiri. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo
Waandishi wa Habari
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo akitoa taarifa kwa wanahabari hii leo ofisini kwake baada ya tukio la mauaji ya watu wawili Jijini Mwanza lililotolea usiku wa kuamkia leo majira ya saa nne usiku eneo la Buzuruga ambapo anaetuhumiwa kutekeleza mauaji hayo ni Mkurugenzi wa Mabasi ya J4 yanayofanya safari zake katika Mikoa ya Mwanza na Mara.

No comments:

Powered by Blogger.