MKUU WA WILAYA YA MAGU ABAINISHA FURSA KUBWA YA UWEKEZAJI ILIYOPO WILAYANI HUMO.
Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Karen Yusun
Na:George GB Pazzo
Wawekezaji kutoka Sekta mbalimbali
nchini wametakiwa kuchangamkia na kutumia fursa ya upatikanaji wa ardhi iliyopo
katika Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, kwa
ajili ya kuimarisha zaidi uwekezaji wao.
Hayo yalisemwa
jana na Mkuu wa Wilaya ya Magu Karen Yusun wakati akizungumzia fursa za uwekezaji zilizopo Wilayani humo na namna zinavyoinufaisha
Wilaya hiyo.
Alisema hadi
sasa makampuni mbalimbali yamejitokeza na kupokelewa vyema kwa ajili ya
kuwekeza katika Wilaya hiyo, huku akiongeza kuwa mbali na makampuni hayo
kunufaika kiuwekezaji, pia yamekuwa yakichangia katika shughuli mbalimbali za
maendeleo ikiwemo kushiriki katika ujenzi wa Maabara pamoja na kutoa ajira kwa
wakazi wake.
“Makampuni
haya yanayowekeza katika Wilaya yetu tumeyapokea vizuri na manufaa yake
tumekuwa tukiyaona maana yamekuwa yakitoa ajira kwa watu wetu, pia yamekuwa
yakichangia katika shughuli za maendeleo ya jamii ikiwemo ujenzi wa Maabara
hivyo nitumie fursa hii kuyashukuru mashirika na makampuni yote ambayo tayari
yamewekeza katika Wilaya yetu”. Alisema Yusun.
Akizungumzia
uwekezaji wa Kampuni ya Mobisol inayojishughulisha na ukopeshaji na uuzaji wa
Mitambo ya kuzalisha Umeme wa jua (Solar) ambayo imeweka Makao Makuu yake katika
Ukanda wa Ziwa Wilayani Magu, Yunus alisema kuwa Kampuni hiyo imeingia wakati
mwafaka Wilayani humo kwa kuwa maeneo mengi ya Wilaya hiyo bado hayana umeme wa
Tanesco hivyo maeneo hayo yatafunaika na nishati ya umeme wa jua kwa ajili ya
matumizi ya nyumbani pamoja na shughuli za kiujasiriamali.
“Kwa kweli
Mobisol wamekuja wakati mwafaka maana kuna maeneo mengi bado hayajafikiwa na
Umeme wa gridi ya Taifa hivyo wahakikishe kuwa wanayafikia maeneo hayo, lakini
pia wananchi watumie vifaa vyao maana umeme ni maendeleo hivyo wanaweza kutumia
vifaa hivyo kuzalisha umeme kwa ajili ya shughuli zao za kiujasiriamali”. Alitanabaisha
Yunus na kuongeza kuwa;
“Wilaya ya
Magu tumepima viwanja kwa ajili ya biashara na uwekezaji wa aina mbalimbali katika
Maeneo ya Kuku Poa, katika Mji wa Kahangara na Kisesa hivyo wawekezaji wawe
tayari kuvinunua viwanja hivyo kwa ajili ya uwekezaji, lakini pia tuko karibu
na jiji la Mwanza ambalo sasa libebanana hivyo waje Magu na tutashirikiana nao vizuri”.
Alidokeza Mhe.Yunus.
Bonyeza Play hapa chini Kusikiliza MAHOJIANO
Bonyeza Play hapa chini Kusikiliza MAHOJIANO
Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Karen Yusun
No comments: