SEHEMU YA PILI: JIFANYIE UCHUNGUZI KATIKA MAMBO YAFUATAYO MAISHANI MWAKO.
2.UDHAIFU
Watu wengi wamekuwa wakishindwa katika maisha yao kwa kushindwa tuu kujua madhaifu yao ni yapi, sehemu ya kwanza ya makala hii tuliongelea kitu kiitwacho UBORA lakini mtu hawezi kuwa bora kila mahali kuna sehemu tuu lazima atakuwa ni mdhaifu.
Sasa usikubali udhaifu fulani uliokuwa nao kwenye jambo fulani ukakusababisha ukashindwa kufikia malengo yako.
Kuna watu wengine wamejikuta wanafanya kazi au mambo fulani pasipo kufanikiwa kwa sababu walishindwa kukaa chini na kuchunguza ni wapi wana udhaifu na ni namna gani wanaweza wakapunguza ule udhaifu maana saa zingine inawezekana ukajifunza mbinu za kuepukana na vitu kadha wa kadha vinavyokufanya uwe dhaifu ila tuu unatakiwa ufahamu kwamba inahitajika nidhamu ya hali ya juu katika hili.
Nataka nikuambie hivi, hakuna binadamu awaye yeyote ambaye hana udhaifu fulani. Kila mtu anao udhaifu katika eneo fulani na sijui kama utakuwa ni binadamu wa kawaida kama hutakuwa na udhaifu fulani, maana biashara nzima ya mafinikio ni kupanda juu ya kosa au makosa fulani siyo kufanikiwa tuu ingekuwa hatuna madhaifu basi hakunge kuwepi na shida ya aina yoyote ile duniani.
Nakumbuka kuna mwalimu wangu alinifundisha kwamba ili uweze kupata mafanikio unatakiwa ufanye mambo ambayo watu walioshindwa kufanikiwa hawayafanyi. Sasa ni mambo mengi ni wewe kujifunza na kuyafanyia kazi.
Moja kati ya mambo ambayo masikini hawayafanyi ni kujiongezea maarifa kila siku, kujifunza kwenye makosa,kubadili mtazamo namna wanavyoona na kuchukulia mambo pamoja na kubadili marafiki ambao hawana mchango katika maisha yao n.k
Lakini pia baada ya kujua madhaifu yako usikate tamaa na kusema mimi ni dhaifu siwezi kufanya hili na lile maana watu wengine huishia hapa na kusema bwana mimi siwezi lakini huwa wanasahau kitu kimoja cha msingi ambacho leo nataka nikukumbushe bure, kwamba kama wewe ni dhaifu katika suala fulani kuna mtu mwingine ni bora katika suala ilo.
Maana yake ni kwamba mnaweza mkaungana na kutengeneza timu ambayo ni nzuri maana atafunika yale madhaifu yako na hii sio kwenye biashara tu ni mpaka kwenye kuoa. Hebu angalia habari hii Bill Gates wakati ameanza kuingia katika ulimwengu wake wa kuandika programu mbalimbali aligundua kwamba ni mdhaifu wa kuongea mbele za watu.
Lakini alijua kwamba ni bora kwenye kuandika programu kwa hiyo hakupoteza mda wake kuangalia udhaifu aliokuwa nao bali alikaa chini akafikiri ni nani rafiki yangu ambaye ni mzuri kwenye kuongea na kutafuta masoko ya vitu .
Akapata jibu kwamba rafiki yake anayeitwa Steve Ballmer ni mzuri katika hili kwa hiyo akamfuata na kumshawishi watengeneze timu ya pamoja wafanye kazi sasa wote mnajua Bill Gates kipindi anaanza hii michaka aliacha chuo akamshawishi na Billmer nae pia akaacha chuo wakaungana leo hii ile timu walioitengeneza kwenye kufanya kazi imewaletea mafanikio makubwa na ya ajabu ambapo wamekuwa Mabilionea japo siku za nyuma kidogo Ballmer alijiuzulu kuwa mkurugenzi mtendaji wa Microsoft.
Kuna siku nilisema, usihangaike kutoboa mwenyewe kwani itakuchukua muda sana hivyo jifunze katika hili. Kuna sheria moja inaitwa sheria ya polarity, hii inasema kwamba kila kitu unachokiona katika dunia hii kina kinyume chake, kwa mfano kinyume cha kulia ni kushoto, mbele ni nyuma, tajiri ni masikini, kukua ni kudumaa na huwezi ukawa katika pande zote mbili kwa wakati mmoja, kwa hiyo katika hayo madhaifu yako tumia hii sheria ya polarity kuyatatua.
Hebu soma walau kwa kiasi kidogo mfano wa watu wanaotaka kuoa;
Kama unataka kuoa tafuta mtu ambaye unaona anaweza kufunika mapungufu uliyokuwa nayo. Kama wewe hujachangamka tafuta aliechangamka ili watu wasije wakaja kwenu wakasema ile familia ni ya mabubu sasa wewe huongei unaoana tena na asieongea hivi upoje wewe?
Pia kama wewe ni mkali wa hasira tafuta mpole kwani ukitafuta mkali kama wewe ndani kukitokea kutokuelewana nani atashuka chini na kumwambia mwenzake yaishe, hapo mke au mume mtaishia kupigana na kuibua ugomvi usioisha katika familia.
Itaendelea...
IMEANDALIWA NA LIFE SECRETS COMPANY YA JIJINI MWANZA AMBAO NI WATAALAMU WA AFYA NA MAENDELEO BINAFSI.
No comments: