LIVE STREAM ADS

Header Ads

SEHEMU YA KWANZA: JIFANYIE UCHUNGUZI KATIKA MAMBO YAFUATAYO MAISHANI MWAKO.

1.UBORA.
Tunaposema mtu anajijua tunamaanisha anafahamu ubora na uwezo alionao katika kufanya mambo mbalimbali,mtazamo aliokuwa nao pamoja na upekee aliokuwa nao pindi akiwa anaishi. 

Kwa bahati mbaya sana watu wengi huwa hawajui ubora wao. Pengine wanaweza wakajua lakini ile hali ya kutokujiamini inawafanya kutokutumia kile ambacho wanakuwa nacho ndani.

Unajua kama unataka kufanikiwa sana ni lazima ujue wewe ni bora katika nyanja zipi ndipo uchukue hatua madhubuti zitakazokupelekea kufanikiwa katika nyanja hizo. Kwa mfano unaweza ukawa ni mtangazaji, mwimbaji, muhamasishaji, mwalimu, mshauri, mtumishi, mwanamichezo n.k.

Pia ni muhimu kujiamini katika kile kitu ambacho unaamini kwamba wewe ni bora, usiogope jiamini kuwa tayari kukifanya mbele za watu kuna msemo unaosema woga wako ndio umaskini wako. 

Sasa unapoogopa kuonesha kile ulichokuwa nacho jua kwamba hakuna ambaye anaweza kugundua hicho ulicho nacho, na hata kama ni msaada fulani angeweza kukusaidia basi hatoweza kukusaidia maadamu hujaonesha kile ulichokuwa nacho na msaada kama nlivyowahi kusema unaweza ukawa ni ushauri, kukusomesha elimu fulani, kukupatia fedha, na pengine kukuunganisha na watu fulani ambao wangekuinua katika hicho ulicho nacho.

Saa zingine unaweza usigundue ubora uliokuwa nao lakini mtu mwingine wa pembeni akaugundua na akakwambia pindi ukikutana nae na akakuambia wewe unaweza kufanya kitu fulani, msikilize na kakifanyie kazi saa zingine Mungu huwa anatumia watu kutuambia tufanye nini ili tuweze kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Na hapa namkumbuka mwanariadha maarufu duniani kutokea Jamaika anaeitwa Ussain Bolt yeye alikuwa anaamini kwamba kipaji chake ni kucheza mpira na hakuwahi kufikiria kwamba yeye ni mwanariadha kwa hiyo alipoteza mda wake mwingi kwenye mpira lakini kila mara baba yake mzazi alikuwa akimwambia Ussain my son "you are not meant for the ball you are meant for running" akimaanisha mwanangu wewe sio mcheza mpira wewe ni mwanariadha baada ya muda mrefu kupia Usain aliamua kujiingiza kwenye riadha na mpaka saivi tunajua binadamu anaekata upepo kuliko wote duniani ni Usain Bolt na amevunja rekodi zote zilizowahi kuwekwa na wanariadha waliopita.

Ussain Bolt ana mafanikio makubwa sana na ni miongoni mwa wanamichezo wanaolipwa fedha nyingi kuliko wote duniani. Nunua kitabu chake kinachoitwa Fast like Lightning utajifunza mengi kutoka kwake ni kitabu kizuri sana.

Ubora uliokuwa nao utakupa uwezo wa juu katika kukufanikisha kwenye hicho unachokifanya na kutumia fursa ambazo zinazokuzunguka.

Hebu kaa chini chukua peni na diary yako andika ubora uliokuwa nao ni sehemu zipi unajiona wewe ni nguli? Diamond alijigundua ni bora katika muziki na wengine wengi kama Jay Dee, Prof J, Linex, nk, 

Lakini pia James Mwang'amba, McLuvanda na Eric Shigongo wamegundua ni bora katika kuhamasisha na kufundisha watu mambo mbalimbali ambayo yanaweza kubadilisha maisha yao kwa kiasi kikubwa. 
Itaendelea...
IMEANDALIWA NA LIFE SECRETS COMPANY YA JIJINI MWANZA AMBAYO NI WATAALAMU WA AFYA NA MAENDELEO BINAFSI.
Email: allnhumph@gmail.com Phone: 0689452670/0765536842

No comments:

Powered by Blogger.