LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANAHABARI WAPANIA UBINGWA PEPSI KOMBE LA MEYA 2015 JIJINI MWANZA.

NA OSCAR MIHAYO, Mwanza
Maandalizi ya mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2015 yameanza kupamba moto ambapo mratibu wa Timu ya wanahabari Edwin Soko amewataka wanahabari wenye uwezo wa kusakata soka wajitokeze kuchukua fomu kwa ajiri ya usaili wa mashindano hayo ambayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi julai 19 mwaka huu.

Mashindano hayo ambayo ni msimu wa tatu mwaka huu tangu kuanzishwa kwake yanaratibiwa na Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula china ya Udhani wa Kampuni ya SBL inayotengeneza Vinywaji jamii ya Pepsi yamenuia kuibua vipaji vya soka na kuviendeleza ikiwa ni pamoja na kuongeza fursa ya ajira kwa vijana.

Akizungumzia mashindano hayo jana, Soko alibainisha kuwa wanataka jamii itambue kuwa wanahabari sio watu wakubeba camera tu na badala yake wana fani na ujuzi mwingine kama kusakata kabumbu.

“Wanahabari sio watu wakubeba makaratasi tu bali tuna vipaji vingi ikiwemo kusakata kabumbu na kuonyesha soka safi na naomba timu pinzani zijiandae kunyolewa kwani maandalizi mwaka huu ni makubwa na sasa tunajinoa vya kutosha’’alisema Soko.

Soko aliongeza kuwa kwa mjibu wa kanuni za mashindano hayo, timu inabidi isajili wachezaji 25 tu ambapo aliwataka wanahabari kujitokeze mapema zaidi ili wasije wakakosa nafasi kwani Mwanza nzima imejaa wanahabari wenye vipaji. 

'Timeisha ongea na kocha mzuri ambae ni Almasi Moshi na kuhaidi kupunguza changamoto kubwa zilizojitokeza mwaka jana jambo litakalo leta hamasa ya ushindani kwenye mashindano hayo".Alisema Soko. 

Tayari mchujo watimu Saba zitakazouungana na timu 14 zilizomaaliza nafasi za juu katika Msimu uliopita wa mashindano hayo umeanza katika viwanja vya Mabatini Jijini Mwanza ambapo jumla zitakamilika timu 25 ambazo zinatarajia kushiriki katika masindano hayo.

No comments:

Powered by Blogger.