LIVE STREAM ADS

Header Ads

HII NDIYO NJIA YA KIPEKEE ILIYOBUNIWA ILI KUENDESHA KAMPENI YA UZAZI WA MPANGO MKOANI KIGOMA.

Na:Mwandishi Wetu
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wadau wa Sekta ya afya, wanatarajia kuendesha Kampeni ya Uhamasishaji Uzazi wa mpango kwa jamii katika maeneo ya mabaa na vilabu vya pombe Mkoani Kigoma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Kigoma Meneja Mawasiliano wa Shirika la World Lung Foundation, Victoria Marijani alisema kuwa mkakati huo, unalenga kufikia malengo ya kitaifa ya asilimia 60 ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma, Dokta Leonard Subi alisema kuwa bado kuna uelewa mdogo wa wakazi wa Mkoa huo katika kujua elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya njia za uzazi wa mpango, kwani kwa sasa ni asilimia 14 ya wakazi hao wanaotumia njia hizo.

No comments:

Powered by Blogger.