LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHADEMA WAZIDI KUITESA CCM MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia
Siku chache baada ya kutangazwa kwa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, baadhi ya wanachama wa chama hicho kutoka Kata ya Kahama Mjini wamejiunga na Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA.

Jana Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kahama Juma Protasi alieleza kuwa wanachama zaidi ya 50 wamejiunga na chama chake akiwemo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ushetu Isaya Bukakiye na kwamba wamekwisha kabidhiwa kadi.

Alisema kuwa wengine waliorudisha kadi za CCM ni pamoja na mabalozi 12 kutoka Kahama Mjini, Mwenyekiti wa CCM Tawi la Majengo na wafuasi wengine wanaendelea kujiunga na Chadema kutokana na kile wanachokieleza kuwa ni mizengwe iliyotumika katika uchaguzi wa kura za maoni ndani ya chama chao.

Katika hatua nyingine Protas alisema kuwa Chadema inaendelea kuimarisha ngome zake na ikiwemo kuandaa mazingira ya ushindi ndani ya majimbo yote matatu ambayo ni Ushetu, Kahama Mjini pamoja na Msalala.

No comments:

Powered by Blogger.