LIVE STREAM ADS

Header Ads

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC YATOA RATIBA YA WANANCHI KUHAKIKI TAARIFA ZAO.

Na:George GB Pazzo
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetoa ratiba kwa wananchi wote waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) kujitokeza katika vituo walivyojiandikishia ili kuhakiki taarifa zao ambapo daftari la mpiga kura limebandikwa.

Zoezi hilo lilianza jana  tarehe Saba mwezi wa Nane katika Mikoa ya Njombe, Iringa, Mtwara, Lindi, Ruvuma, Katavi, Rukwa, Mbeya, Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma, Kagera, Simuyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Morogoro ambapo litafikia tamati tarehe 11 mwezi huu wa nane.

Kuanzia tarehe 11 mwezi huu itakuwa katika Mikoa ya Pwani na Zanzibar ambapo zoezi hilo litafikia tamati tarehe 15 mwezi huu wa nane na Mkoa wa Dar es salaam itakuwa ni kuanzia tarehe 13 mwezi huu hadi tarehe 17 mwezi huu.

Taarifa iliyotolewa na NEC imefafanua kwamba Mashine zitakuwepo katika Ofisi za Watendaji wa Kata kwa ajili ya kusahihisha makosa yaliyojitokeza  wakati wa kujiandikisha na inawahimiza wananchi waliohama wakahakikishe taarifa zao mahali watakapopigia kura katika uchaguzi wa Mwaka huu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25 mwaka huu.

NEC inasema "Tunza Kadi Yako, Usimpe Mtu. Jitokeze, Nenda Kahakiki Taarifa Zako".

No comments:

Powered by Blogger.