WAJASIRIAMALI MKOANI MWANZA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO ILI KUKUZA MITAJI YAO.
Afisa Mikopo kutoka Sakosi ya Utoaji Mikopo kwa Wajasiriamali nchini ya Take and Back Financial Insitution Neema Joseph Jingu (Kushoto) akizungumza na GB Pazzo (Kulia) katika Ofisi za Sakosi hiyo zilizopo Jengo la CCM Mkoa wa Mwanza.
Na:George GB PazzoWajasiriamali Mkoani Mwanza wameshauriwa kuchangamkia fursa za Mikopo zinazotolewa na taasisi mbalimbali za kifedha hapa nchini, kwa ajili ya kukuza mitaji ya biashara zao.
Ushauri huo ulitolewa jana na Afisa
Mikopo kutoka Sakosi ya Utoaji Mikopo kwa Wajasiriamali nchini ya Take and Back
Financial Insitution Neema Joseph Jingu wakati akizungumza na Radio Metro katika ofisi za Sakosi hiyo zilizopo Jengo la CCM Mkoani Mwanza.
Jingu alisema kuwa Wajasiriamali wanapaswa
kuondokana na hofu ya kujitokeza kukopa katika taasisi hizo, kwa kuwa hatua
hiyo itawasaidia kukuza biashara zao.
“Taasisi nyingi za fedha nchini ikiwemo Sakosi
ya Take and Back Financial Insitution hutoa elimu ya Ujasiriamali kabla ya
kutoa mikopo yake kwa wajasiriamali, jambo ambalo limesaidia wakopaji kumudu kurejesha
mikopo yao kwa wakati”. Alibainisha Jingu.
Aidha alibainisha kuwa zaidi ya Wajasiriamali
400 wamenufaika na Sakosi hiyo Mkoani Mwanza, tangu kuanzishwa kwake mwezi
Septemba Mwaka jana.
Hata hivyo baadhi ya Wajasiriamali waliozungumza
na Radio Metro Jijini Mwanza, walisema kuwa bado taasisi za fedha zinazotoa
mikopo kwa Wajasiriamali zina masharti magumu yanayosababisha kutonufaika na
mikopo hiyo ambapo wameomba kupunguzwa kwa baadhi ya masharti hayo ambayo ni
pamoja na riba kubwa sanjari na uhitaji wa hati ya nyumba ama kiwanja.
“Mimi kinachonichanganya kabisa katika hii
mikopo ni kuanza kuulizwa hati ya nyumba au kiwanja wakati hauna. Hivyo mimi
ningeomba hivyo vigezo wavipunguze”. Alisema kijana Benjamin Zacharia ambae ni
mwenyeji wa Wilaya ya Misungwi anaefanya shughuli zake za ujasiriamali Jijini
Mwanza.
Kwa pamoja Bi.Tatu Mussa pamoja na Kijana Rio
Michael ambao ni Wajasiriamali Jijini Mwanza alisema riba kubwa, leseni, hati
ya nyumba ama kiwanja pamoja na mirorongo mingine isiyo na tija inapaswa kuondolewa
kwa wajasiriamali maana inazidi kuwadidimiza wajasiriamali.
Afisa Mikopo kutoka Sakosi ya Utoaji Mikopo kwa Wajasiriamali nchini ya Take and Back Financial Insitution Neema Joseph Jingu.
Afisa Mikopo kutoka Sakosi ya Utoaji Mikopo kwa Wajasiriamali nchini ya Take and Back Financial Insitution Neema Joseph Jingu.
Special Thanks to Radio Metro Fm.
No comments: