LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MWANZA WAANZA KWA MAHUDHURIO HAFIFU.

Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Vyama vya Waandishi wa Habari nchini UTPC Abubakar Karsan akizungumza katika Mkutano Mkuu wa mwaka 2014 wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza (Mwanza Press Club-MPC) unaofanyika leo Septemba 12,2015 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Kulia ni Jilala Calvin ambae ni Mjumbe Kamati Tendaji MPC.
Na:Binagi Media Group
Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza (Mwanza Press Club-MPC) kwa mwaka 2014 umeanza hii leo katika Ukumbi wa Halmshauri ya Jiji la Mwanza kwa mahudhurio hafifu ikilinganishwa na mahudhurio ya mkutano wa mwaka 2013.

Kwa kawaida Mkutano Mkuu wa MPC unapaswa kufanyika mwezi wa pili kila mwaka lakini kutokana na sababu mbalimbali, kumekuwepo na ucheleweshaji wa kufanyika kwa mkutano huo.

Kumbuka Mkutano huo mwaka huu unafanyika kwa umhimu mkubwa ikizingatiwa kwamba ni mwaka ambao MPC inafanya Uchaguzi wake Mkuu wa Kuwapata Viongozi wake watakaokuwa madarakani kwa miaka mingine mitatu ijayo.

MPC ina zaidi ya wanachama 124 na twakwimu za mkutano wa mwaka 2013 zinaonyesha kuwa wanachama 59 walihudhuria Mkutano Mkuu huku wanachama 46 wakishindwa kuhudhuria huo na wanaosalia wakiwa hawajulikani kama ni wanachama hai ama la.

Katika uchaguzi wa uongozi unaomaliza muda wake Deus Bugaywa kuwa Mwenyekiti, Denis Mpagaze Makamu Mwenyekiti na Jimmy Luhende Katibu Mkuu pamoja na viongozi wengineo. Jambo la kusikitisha ni kwamba viongozi hao nao hawajahudhuria Mkutano wa Mwaka huu hadi dakika hii.
Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza Edwin Soko
Jilala Calvin ambae ni Mjumbe Kamati Tendaji MPC.
Wajumbe wa MPC
Wajumbe wa MPC
Wajumbe wa MPC
Wajumbe wa MPC
Wajumbe wa MPC
Adolf Stakulimwa ambae ni Mkaguzi Matekelezo kwa Mikoa ya Mara na Simiyu kutoka Mfuko wa Hifadhi za Jamii LAPF akizungumza na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza MPC katika Mkutano Mkuu wa chama hicho mwaka huu na kutoa semna juu ya mfuko huo.

No comments:

Powered by Blogger.