LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAWILI WAPOTEZA MAISHA KATIKA MACHIMBO YA MCHANGA MKOANI KAGERA.

Na:Elisa Anatory, Kagera
Watu wawili wakazi wa Kata ya Kanyangeleko, Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mchanga.

Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa tano asubuhi Katani humo ambapo mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa kifusi hicho kilibomoka kutokana na watu kutofuata utaratibu wa kuchimba katika eneo hilo.

Walisema juhudi za kuokoa maisha yao ziligomga mwamba kutoka na waokoaji kuchelewa kupata taarifa, kwani uokoaji ulianza majira ya saa nane mchana ambapo tayari walikuta watu hao wamefariki dunia.

Waliopoteza maisha wametambuliwa kwa majina ya Nelson Johanes pamoja na Samadu Rashid wote wakiwa ni wakazi wa Manispaa ya Bukoba.

Akizungumzia tukio hilo, Afisa Madini Mkoa wa Kagera Ally Said amewata wachimbaji wa Mchanga Mkoani humo  kufanya shughuli zao kwa kuzingatia taratibu za kiusalama na hali ya hewa hususani katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.

No comments:

Powered by Blogger.