LIVE STREAM ADS

Header Ads

CCM KAHAMA WATUMBUANA.

Na:Shaban Njia
Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, kimewasimamisha uanachama zaidi ya wanachama 135 kutokana na tuhuma za kukihujumu chama.

Uamuzi huo umetolewa juzi katika Kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya  ya Kahama na Katibu wa Chama hicho Alexandrina Katabi na kuongeza kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kuona mapungufu katika kata mbalimbali na kuongeza kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na wanachama wengine kuwajibishwa katika matawi yao.

Katabi alisema kuwa baadhi ya Wanachama walioachishwa ni pamoja na Mabalozi 20, Makatibu uenezi, uchumi na fedha 60 huku wengine 20 wakipewa onyo kali.

Aliongeza kuwa wenyeviti wa Vitongoji watano wamepewa onyo kali, wenyeviti 10 wa Serikali za Vijiji wametimuliwa huku 20 wakipewa onyo kali.

No comments:

Powered by Blogger.