SUALA LA WAFUNGWA KUNYONGWA, SERIKALI YATOA KAULI.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Harrison Mwakyembe (Kulia) akizungumza katika kikao baina yake na watendaji wa wizara yake Mkoani Mwanza.
Kutoka Kushoto waliokaa ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ndaro Kulwijira, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana (Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza) Baraka Konisaga.Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Serikali imesema bado haijafikia uamuzi wa
kutekeleza hukumu ya kunyonga wafungwa, wanaohukumiwa kunyongwa hadi kufa
kutokana na makosa ya jinai ikiwemo mauaji.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison
Mwakyembe, alitoa kauli hiyo jana Jijini Mwanza, wakati akizungumza na Watendaji wa
idara mbalimbali za Serikali ikiwemo Magereza pamoja na Mahakama, kabla ya
kuanza ziara yake ya kikazi Mkoani Mwanza.
Dkt.Mwakyembe alisema kuwa suala la
kunyonga wafungwa linahitaji maridhiano kwa kuwa utekelezaji wake unaweza kuliingiza
taifa katika migogoro isiyo ya lazima ikizingatiwa kwamba watetezi wa haki za
binadamu pamoja na wanaharakati mbalimbali wamekuwa wakilipinga.
Katika hatua nyingine Dkt.Mwakyembe
alikemea vitendo vya ukatili na mauaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambalo
limeshamiri katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa huku Mkoa wa Mwanza ukiwa kinara
ambapo amesema Serikali haiwezi kukubali vitendo hivyo kuendelea kujitokeza.
Sikiliza Sauti HAPA Au Play Hapa Chini
No comments: