LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA ANYOFOA 51 KUTOKA UKAWA MKOANI ARUSHA.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (mwenye shuka jekundu) akiwasili eneo la mkutano wa hadhara katika kata ya Albalabal wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha. 

Ilikuwa juzi ambapo Shaka alihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata hiyo ikiwa ni katika kuhitimisha ziara yake Wilayani ngorongoro. Mkutano huo ulikuwa wa aina yake kwani uliwavuta ndani ya chama vijana wapya zaidi ya 51 kutoka Ukawa ambao walipokea kadi mpya za CCM.
Kaimu katibu Mkuu pamoja na viongozi alioongozana wakisaini vitabu vya wageni
Diwani wa Kata ya Albalbal Ndg:Emmanuel Gabriel Tonge Akihutubia kwa kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu Shaka H Shaka katika kata ya Albalbal
Pia katika ziara hiyo Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka aliweza kupokea wanachma wapya zaidi ya 51 katika kata ya Albalbal
Baadhi ya Wanachama wapya wakila kiapo cha chama

Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka akivikwa shuka la kimila ikiwa ni ishara ya kupokelewa na Wananchi wa Kimasai katika kata hiyo
Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka akicheza nyimbo ya kimasai pamoja na Wananchi wa kata ya Albalbal
Kaimu Katibu UVCCM Taifa, Mkuu Shaka Hamdu Shaka akihutubia Wananchi wa Kata hiyo
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka akihutubia Wananchi wa Kata Ya ALBALBAL, Ngorongoro Mkoani Arusha.
Wananchi wa Kata ya Albalbal, Ngorongoro Mkoani Arusha, wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu  Uvccm Taifa kwa umakini.
Imeandaliwa na Fahad Siraji

No comments:

Powered by Blogger.