LIVE STREAM ADS

Header Ads

MGANGA WA JADI MBARONI MKONI KIGOMA KWA TUHUMA ZA UBAKAJI.


Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
Jeshi la Polisi mkoani  Kigoma  linamshikilia Hamza Saidi,(40) mganga wa jadi, mkazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji, kwa tuhuma za kumbaka binti mwenye umri wa miaka (20) aliyefika nyumbani kwake kupata tiba.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma SACP.Fredinandi Mtui, amesema tukio hilo lilitokea mei jana na kwamba mtuhumiwa amekwamatwa kwa ajili ya uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabiri kabla ya kufikishwa mbele ya sheria.

No comments:

Powered by Blogger.