LIVE STREAM ADS

Header Ads

RIPOTI KUTOKA HOSPITALINI JUU YA JAMAA ALIEJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU JIJINI MWANZA.

Hali ya kiafya ya kijana Paul Paschal (40) baba wa watoto wawili ambae jana alijirusha kutoka katikati ya mnara wa simu uliopo katika barabara ya Makongoro-Airport Jijini Mwanza inaendelea vizuri.
Na BMG

Hayo yamesemwa na Heresi Madatta ambae ni muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure, aliempokea kijana huyo na kuongeza kwamba kijana huyo hakupata madhara makubwa ikiwemo kuvunjika viungo vya mwili.

Taarifa za awali zilionyesha kuwa kijana huyo alikumbwa na tatizo la ugonjwa wa malaria ambayo ilipanda kichwani na kusababisha kupanda juu ya mnara huku akitishia kujirusha chini kutokana na ugumu wa maisha.

Hata hivyo duru za habari zinaeleza kwamba si mara ya kwanza kijana huyo ambae anadaiwa kuwa ni mtumiaji wa dawa za kulevya ikiwemo kunusa gundi kupanda juu ya minara na kutaka kujiua.
Bonyeza HAPA Kutazama Picha

No comments:

Powered by Blogger.