SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI NCHINI KUANZA UTUMBUAJI MAJIPU.
Call 0688 447 444 Or 0767 68 28 88
Judith Ferdinand na Getruda Ntakije,Mwanza
Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA), limesema linaunga mkono juhudi za utumbuaji majipu, zinazofanywa na rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA), limesema linaunga mkono juhudi za utumbuaji majipu, zinazofanywa na rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti Taifa wa SHIVYATIATA, Abdulrahman Lutenga, ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza, wakati katika ziara ya kutembelea mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni katika kutekeleza zoezi la kuchagua viongozi wa shirikisho hilo katika Wilaya na Mikoa yote nchini.
"Tunaungana na rais Magufuli kuyatumbua majipu yote yaliyopo katika tasnia nzima ya tiba asili hapa nchini hivyo hatuko tayari kuona agizo la usajili linapuuzwa". Alisema Lutenga.
No comments: