LIVE STREAM ADS

Header Ads

AFARIKI AKIWA KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI MKOANI SHINYANGA. TAARIFA ZAKE ZAKANGANYA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shaban Njia
Mwanaume mmoja amekutwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wangeni ya Nyanda Geust House iliyopo Mtaa wa Manyovu Kata ya Majengo katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Taarifa zinaeleza kwamba mwanaume huyo ni mkazi wa Kijiji cha Pemba Wilaya ya Tarime Mkoani Mara na amaejulikana kwa jina la Chacha Marwa Mwaiseko anaekadiriwa kuwa na miaka 37 na 40.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Mika Nyange, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo lilitokea juzi katika nyumba hiyo ya kulala wageni.

Aidha Kamanda Nyange alisema kuwa marehemu wakati wa upekuzi alikutwa akiwa  na pesa kiasi cha shilingi elfu saba mia tisa (7,900) na risti ya pombe kutoka Silwa Pub ya Jijini Mwanza ambapo inaonyesha alikuwa amekunywa kinywaji cha bia aina ya balimi.

Kamanda Nyange amesema kitambulisho cha kupiga kura cha marehemu kilionyesha jina lake ni Samweli Paulo mkazi wa Sengerema mkoani Mwanza huku kitabu cha wangeni akiwa ameandika jina la Chacha Marwa mkazi wa kijiji cha Pembe wilayani Tarime.

Ametoa wito kwa wananchi kuwa wakweli katika kuandikisha majina yao pindi waendapo ugenini (nyumba za kulala wageni) na mahali sahihi wanapotoka ili kuondoa usubufu pindi matatizo yanapotokea.

“Mimi niliogopa sana mtu amelala hata hasituki ndipo niliomba msaada kwa wateja wengine waliopanga katika Nyumba hii na pia kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ndipo walipofika na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika hospitali ya Wilaya”. Amesema Pili Masanja ambae ni mhudumu wa nyumba ya kulala wangeni ya Nyanda Geust house.

Mwili wa marehemu umeifadhiwa katika hospital ya Wilaya ya Kahama kwa uchuguzi zaidi huku wakisubiriwa ndugu wa marerhemu kuuchukua kwa ajili ya mazishi.

No comments:

Powered by Blogger.