KANISA LA SINZA CHRISTIAN CENTER LA JIJINI DAR LATUPIWA VYOMBO NJE.
Kutokana na kudaiwa deni la zaidi ya milioni 100 Kanisa la Sinza Christian Center la Jijini Dar es salaam, limetupiwa nje vyombo vyake na dalali aliyepewa tenda hiyo, aliefahamika kwa jina moja la Joshua ambae alipewa idhini na Mahakama pamoja na mmiliki wa jengo hilo, Prosper Rwendera.
Akizungumza na Dar es salaam yetu Blog, mke wa mmiliki wa jingo hilo, Patricia Prosper, amesema; “huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu".
Alipotafutwa msemaji wa Kanisa hilo ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotakiwa kuzungumza walikataa kwa madai kuwa hawana mamlaka ya kuzungumza lolote kuhusiana na sakata hilo.
Viti vyote vikiwa vimetolewa nje
Vyombo vya Muziki vikiwa nje
Magari yakiwa yanatolewa nje
Vitu vikiwa nje ya Jengo hilo ambapo mpaka sasa kuna sinto fahamu vinapelekwa wapi
Vikombe nje
Wametoa vitu vyote
Baadhi ya Magari yaliyotolewa katika Jengo hilo ambapo hapo awali ilikuwa ni Kanisa
Kushoto kwa mbali ni Mke wa Miiliki wa Jengo hilo Bi. Patricia Prosper akiendelea na majukumu huku pembeni vijana wakipata maelekezo ya kuendelea kutoa vitu.
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa
No comments: