LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA JIJINI MWANZA ATUPWA GEREZA.

Na BMG

Mahakama ya Mwanzo Mkuyuni iliyopo Jijini Mwanza, imemhukumu Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugando B, Juma Richard Masanja (CUF), kifungo cha miezi sita gerezani, kwa kosa la kutishia kuua mama na familia yake.

Akitoa hukumu hiyo jana katika kesi ya jinai nambari 405 ya mwaka 2016, hakimu wa Mahakama hiyo, Mhe.Mwambeleko, alisema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo june nane mwaka huu majira ya saa mbili usiku katika Mtaa wa Bugando B, ambapo alitishia kumuua mkazi wa mtaa huo, Bi.Consolatha George pamoja na familia yake.

"Ni kosa kutishia kuua kwa maneno kwani ni kinyume na kifungu cha 89 cha sheria ya kanuni za adhabu". Alisema Mhe.Mwambeleko na kutanabaisha kwamba hukumu hiyo ni fundisho kwa mshtakiwa ambae ni kiongozi pamoja na viongozi wengine wenye kutumia mabavu dhidi ya wananchi. 

No comments:

Powered by Blogger.