LIVE STREAM ADS

Header Ads

SABABU ZA UTEUZI WA MKUU WA WILAYA YA IKUNGI KUTENGULIWA NDANI YA SAA 24 ZAWEKWA BAYANA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Dkt.John Joseph Pombe Magufuli.

June 27 mwaka huu ikiwa ni siku moja baada ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kufanya uteuzi wa wakuu wa Wilaya nchini pamoja na Wakuu Mikoa watatu ambao ni wapya, zilizagaa taarifa mitandaoni kwamba uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Fikiri Avias Said, umetenguliwa na nafasi hiyo imechukuliwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu.

Hii leo taarifa zimethibitishwa na Dkt.Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam katika hafla ya kuwaapisha Wakuu wapya wa Mikoa walioteuliwa iliyoambatana na zoezi la Kula Kiapo cha Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Wakuu wa Wilaya ambapo amesema jina la Mkuu wa Wilaya ya Ikungi lilikosewa na kwamba Mkuu wa Wilaya ya Ikungi halali ni Miraji Mtaturu.

Jumapili iliyopita June 26, Rais Magufuli aliwateua Wakuu wa Wilaya zote 139 nchini ambapo 100 ni wapya katika awamu yake na 39 wakiwa ni wale walioingia madarakani tangu awamu iliyopita huku Wakuu wa Mikoa ya Mara, Ruvuma na Shinyanga wakiwa ni wapya.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza, ambae ni Mkuu Mpya wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu.

No comments:

Powered by Blogger.