LIVE STREAM ADS

Header Ads

UJUMBE MAALUMU KUELEKEA SIKU YA KIMATAIFA YA KUONGEZA UELEWA KUHUSU WATU WENYE UALIBINO.


Katika kuelekea katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuongeza Uelewa dhidi ya Watu wenye Ualbino (International Albinism Awareness Day) yatakayofanyika tarehe 13/06/2016,

Mimi Suleiman Magoma, mtanzania mwenye Ualbino  pamoja na tovuti yangu yawww.albinismtanzania.co.tz tumeandaa video clip fupi(kama inavyoonekana hapo juu)  yenye kutoa Elimu ya Albinism  kwa jamii ya Watanzania wenzetu ili wawe na uelewa wa kutosha na hatimae  kuachana na dhana,fikra na mitazamo potofu kuhusu sisi  watu wenye Ualbino.

Ewe mtanzania mwenzangu naomba uniunge mkono kwa kusambaza hii Video Clip pamoja na caption yake kwa ndugu jamaa,marafiki,vyombo vya habari, ma group  mbalimbali ya whatsapp pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii  ili elimu hii iweze kuwafikia watu wengi na hatimae utakuwa umesaidia sana kupunguza au kukomesha kabisa vitendo vya Ukatili,Unyanyapaa na Mauaji ya Watu wenye Ualbino katika nchi yetu. Tushirikiane katika kuhakikisha Elimu ya Albinism inawafikia watu kadri inavyowezekana.
Suleiman Magoma
+255 766 467960
Suleiman.magoma41@gmail.com
www.albinismtanzania.co.tz

No comments:

Powered by Blogger.