LIVE STREAM ADS

Header Ads

BABA ANAEMUANDAA MWANAE KUWA RAIS WA TANZANIA MWAKA 2050 AZUNGUMZA NA BMG.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mzee Mohamed Nasoro kutoka mkoani Singida ambae ni mkereketwa na mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM ambae amewasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli kwa kazi yake nzuri anayoifanya.

Mzee Nasoro ambae alitoka Singida Julai 20,2016 kwa usafiri wa baiskeli aliwasili mkoani Dodoma Julai 22,2016 akiwa ameambatana na mtoto wake, Yusuph Mohamed Nasoro (2) ambae anaandaliwa na mzee huyo ili kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2050.

Mzee Naoso anasema alifika na mtoto huyo mkoani Dodoma ili ashuhudie matukio muhimu ya CCM ikiwemo Mkutano Mkuu Maalumu ambao ulifanyika jana na Wajumbe wa Mkutano huo kumchagua Rais John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kura zote za ndiyo.

"Akiwa na miezi minne na nusu, huyu mtoto kwa maajabu akatamka mimi Rais halafu akafunga mdomo". Anatanabaisha Mzee Nasoro wakati akifafanua sababu za yeye kuanza kumuandaa mtoto huyo kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2050.

Mzee Nasoro amesisitiza juu ya suala la wazazi wote wakiwemo wana CCM kuwaandaa watoto kwa ajili ya kukiimarisha chama kwa miaka ijayo ikiwemo kuwa viongozi wa baadae kwa kuwafunza.
Mzee Nasoro akitoa ufafanuzi kwa BMG juu ya mtoto wake ambae anamuandaa kuwa Rais mwaka 2050
Huu ndio usafiri wenyewe. Hadi tunaenda mitamboni, BMG haijapata taarifa yoyote ikiwa mtoto huyo alibahatika kuonana na Rais Magufuli kama ilivyokuwa dhamira ya Mzee Nasoro kutaka mtoto wake aonane na Rais Magufuli ili ampe Baraka za kuwa Rais mwaka 2050.

No comments:

Powered by Blogger.