LIVE STREAM ADS

Header Ads

DKT.MAGUFULI KUKIIMARISHA ZAIDI CHAMA CHA MAPINDUZI CCM.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti Mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM, ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli (kushoto), akifurahia jambo wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho uliofanyika jana Mjini Dodoma.
Na BMG

Ni katika Mkutano huo ambapo Mwenyekiti Mstaafu ambae pia alikuwa Rais wa awamu ya nne, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, alistaafu Uwenyekiti wa CCM na kumkabidhi uongozi Dkt.Magufuli ambae alichaguliwa kwa kura za ndiyo na wajumbe wote 2,398 wa mkutano huo.

Dkt.Magufuli alisema katika uongozi wake, atahakikisha anaimarisha ustawi wa chama ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama pamoja na kurejesha maadili kwa wanachama ikiwemo kukomesha suala la rushwa hususani nyakati za uchaguzi pamoja na kukomesha suala la watumishi hewa ndani ya chama.

"Naondoka nikiwa najua Chama cha Mapinduzi chini ya Dkt.John Pombe Magufuli kiko salama na kitapata mafanikio makubwa". Alisema Dkt.Kikwete katika hotuba yake ya kuhitimisha uongozi wake ndani ya chama.
Licha ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (pichani) kuandika barua ya kustaafu uongozi wake kama ilivyo ada kwamba Mwenyekiti mpya baada ya kuchaguliwa huteua safu yake ya viongozi, Dkt.Magufuli baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM alimtangaza Kinana pamoja na Sekretarieti yake kuendelea na uongozi.
Christopher Mwita Gachuma, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka mkoani Mara akielekea kuketi ukumbini.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu, wakiwemo kutoka mkoani Mara wakifuatilia Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu, wakiwemo kutoka mkoani Mwanza wakifuatilia Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wakifuatilia Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM wakikubaliana na matokeo yaliyompa ushindi Dkt Magufuli ushindi wa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Wajumbe kutoka mkoani Mwanza, wakiwa katika shangwe
Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa mkoani Simiyu, Luhaga Mpina, akizungumza na wanahabari nje ya Ukumbi wa Dodoma Convetion Center mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Ileme mkoani Mwanza ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, akizungumza na wanahabari nje ya Ukumbi wa Dodoma Convetion Center, ambapo alisema Dkt.Magufuli anastahili kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na kwamba anao uwezo mkubwa wa kukiimarisha chama hicho.
Mbunge wa Jimbo la Ileme mkoani Mwanza ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula (kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wadau.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convetion Center.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka mkoani Mwanza, Flora Magabe (kushoto) akiwa pamoja na Mama Maria Hewa (kulia).
Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa mkoani Simiyu, Luhaga Mpina (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wengine.
Makomredi kutoka mkoani Mwanza, wakiwa nje ya ukumbi wa Mikutano
Wanahabari Dr.Alphonce Tonny Kapela wa Metro Fm Mwanza (kushoto) akiwa na Geoge Binagi-GB Pazzo wa 102.5 Lake Fm Mwanza (kulia).
BMG Live
Mdau wa BMG ambae pia ni Mwanahabari wa Sibuka Fm kutoka Jijini Dar es salaam.

No comments:

Powered by Blogger.