JICHO LA BMG MJINI DODOMA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Hapa ni Independence Garden Mjini Dodoma. Wanahabari kutoka mkoani Mwanza, George Binagi-GB Pazzo wa 102.5 Lake Fm (kulia), Alphonce Tonny Kapela wa Metro Fm (katikati) na Mwenyeji wao, Revocatus Herman kutoka Dodoma wanaendelea kuzunguka katika Mitaa mbalimbali kujionea namna mji wa Dodoma unavyokuwa kwa kasi.
BMG imebaini namna mji wa Dodoma ulivyopangiliwa katika ramani huku suala la usafi likipewa kipaumbele na wakazi wa Dodoma.
Ni mji ambao haujabanana kama ilivyo kwa baadhi ya miji hapa nchini. Kuna kasi ya ujenzi wa makazi na majengo ya uwekezaji kama vile hoteli jambo ambalo linaufanya mji wa Dodoma kupendeza.
Matarajio ya Serikali ya awamu ya tano ni kuhamishia Makao Makuu ya ofisi zote za Serikali mkoani Dodoma. Hakika mji wa Dodoma utatanuka maradufu zaidi.
Msimu huu wa mwezi wa saba, hali ya hewa mkoani Dodoma ni ya maridi hususani majira ya kuanzia saa kumi na moja za jioni na kuendelea.
Sylvester Joseph-Jtz wa Afya Radio ya Jijini Mwanza akiwa Independence Garden Mjini Dodoma.
GB Pazzo wa 102.5 Lake Fm ya Jijini Mwanza akiwa Independence Garden Mjini Dodoma ambapo anakufikishia matukio yote.
Revocatus Herman kutoka Dodoma.
Kumbuka leo Julai 25,2016 ni Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa nchini ambayo Kitaifa yanafanyika Mjini Dodoma, na yataletwa kwenu na BMG ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Amiri Jeshi Mkuu ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli.
Bonyeza HAPA Kwa Picha Zaidi.
No comments: