LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA MSALALA MKOANI SHINYANGA KUHARAKISHA MAENDELEO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shaban Njia
Imetanabaishwa kwamba kupatikana kwa makao makuu ya halmashauri mpya ya wilaya ya Msalala iliyopo wilayani Kahama katika Mkoa wa Shinyanga,  kutafungua fursa nyingi za kimaendeleo  katika halmashauri hiyo.

Hayo yaliezwa jana na baadhi ya wadau wa maendeleo katika halmashauri hiyo kwenye kikao maalum cha kamati ya Ushauri ya Maendeleo ya Wilaya ya Msalala kilichofanyika mjini Kahama.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo, John Mahona, ambaye ni Mtendaji wa kata ya Chella, alisema kutokuwa na uhakika wa wapi makao makuu ya halmashuri hiyo yatakuwa na katika kata gani ni moja kati ya vitu ambavyo vinachangia kutokupatikana kwa maendeleo kwa haraka katika halmashauri ya Msalala.

"Jambo hili na mchakato wa wapi makao makuu ya halmashauri ya Msalala yawe wapi, limekuwa la muda mrefu na kwa sasa lazima jambo hili liishe ili tufanye mambo mengine ya msingi, tunataka kikao hichi kiwe cha muda mfupi na chenye tija". Alisema Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu, mapema wakati akizungumza katika kikao hicho na kuongeza;

Kusipokuwa na marekebisho mengine, imependekezwa kwamba makao makuu ya halmashauri ya Msalala yawe katika Kata ya Ntobo.

No comments:

Powered by Blogger.