LIVE STREAM ADS

Header Ads

MSICHANA WA MIAKA 17 ATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MTOTO MCHANGA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shaban Njia
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, linamshikilia msichana anaefahamika kwa jina la Yorita Godfrey (17), mkazi wa Kijiji cha Kalenge Biharamulo mkoani Kagera kwa kosa la kuiba mtoto mchanga mwenye umri wa miaka miwili.

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, Mika Nyange, amesema tukio hilo lilitokea  kata ya Tarakea Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ambapo mtuhumiwa aliiba mtoto huyo jumapili iliyopita akiwa kanisani na kisha kutoroka nae hadi nyumbani Kahama.

Alisema tuhumiwa huyo alikuwa akifanya kazi za ndani kwa Michael Massawe mkazi wa Tarakea Wilayani Rombo na kuongeza kuwa alikwenda kusali ndipo alipomkuta mtoto huyo nje ya kanisa la Romani Katoliki  wilayani humo akiwa na wenzake wakicheza na kisha kumchukua na kuondoka nae.

Mtuhumiwa huyo amesema alitenda kosa hilo kwa lengo la kutaka kumridhisha mumewe kuwa nae ana mtoto. Anatarajiwa kurejeshwa mkoani Kilimanjaro kujibu shutma zinazomkabiri.

No comments:

Powered by Blogger.