LIVE STREAM ADS

Header Ads

BULAYA NA WASIRA USO KWA USO JIJINI MWANZA KWENYE RUFAA YA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara, Esther Bulaya (kushoto) kwa tiketi ya Chadema, pamoja na wasaidizi wake, wakitoka nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, baada ya hii leo kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu jimboni humo iliyofunguliwa na wapiga kura, wanachama wa CCM kupinga ushindi wake kuahirishwa.
Na BMG
Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Bunda Mjini, Steven Wasira (mwenye suti nyeusi), akiteta jambo na wapiga kura wa jimbo hilo waliofungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana jimboni humo.
Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (kushoto), akifurahia jambo na wakili wa wakata rufaa, Costantine Mtalemwa (kulia), baada ya kesi kuahirishwa.
Wakili wa wakata rufaa, Costantine Mtalemwa (kushoto), wakili wa Bulaya, Tundu Lissu (katikati) na mjibu maombi, Esther Bulaya, wakisalimiana baada ya kesi kuahirishwa.

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imesikiliza rufaa iliyokatwa na wapiga kura wanne wa Chama cha Mapinduzi CCM katika jimbo la Bunda mjini mkoani Mara, kupinga ushindi wa mbunge wa jimbo hilo, Esther Bulaya, kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, katika uchaguzi mkuu mwaka jana.

Wakili wa wakata rufaa, Constatine Mutalemwa, ameiomba mahakama hiyo kuzingatia hoja tatu walizowasilisha ikiwemo tuhuma za vitendo vya rushwa vinavyodaiwa kufanywa na wafuasi wa mbunge Bulaya pamoja na kutofautiana kwa kura zilizopigwa katika baadhi ya vituo na idadi halisi ya wapiga kura walioandikishwa.

Hata hivyo wakili wa mbunge Bulaya,  Tundu Lissu, ameiomba mahakama hiyo kutupilia mbali hoja zote tatu zilizowasilishwa na upande wa walalamikaji kwa kuwa walishindwa kutaja vifungu vya sheria vilivyokiukwa hivyo madai yao hayana msingi.

Lissu pia amesema hoja  inayodai kwamba kulikuwa na vitendo vya rushwa kutoka kwa wafuasi wa Bulaya, haina msingi kwa kuwa ili mahakama imtie hatiani mlalamikiwa ni lazima kuwe na ushahidi wa mtuhumiwa kuamuru au kushuhudia vitendo hivyo.

Jaji wa Mahakama hiyo, Lameck Mlacha, ameahirisha shauri hilo hadi alhamisi iyayo ya agost 25, hukumu ya kesi hiyo itakapotolewa.

No comments:

Powered by Blogger.