MADIWANI HALMASHAURI YA USHETU MKOANI SHINYANGA WAKOMALIA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI HIYO.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na Shaban Njia
Baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga, limeitaka halmashauri hiyo kutofanya mzaha kwenye suala la ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo.
Na Shaban Njia
Baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga, limeitaka halmashauri hiyo kutofanya mzaha kwenye suala la ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo.
Kwa sasa watumishi wa halmashauri hiyo wanaendesha shughuli zao kwa muda katika jengo la ofisi ya Kata ya Nyamilangano Ushetu ambako ndiko makao makuu ya halmashauri hiyo yanatarajia kujengwa.
Hayo yalibainika juzi katika kikawao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika katika Kata ya Nyamilangano wakati walipokuwa wakijadili shughuli mbali mbali za maendeleo katika Halmashauri yao.
Diwani wa viti maalumu Kata ya Bulungwa, Esther Matone, alisema licha ya kuhamia katika makao mapya ya halmashauri hiyo lakini bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa majengo ya ofisi pamoja na miundo mbinu kwa watumishi.
Naye diwani wa Kata ya Sabasabini, Emmanuel Makashi, alimweleza mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Juma Kimisha, kwamba kuna haja ya kutojenga jengo la ghorofa walilo panga kujenga na kujenga jengo la kawaida kama lile waliloliacha huko Kahama ili kuharakisha ujenzi na kudai kuwa mali zilizopo nje zina zaidi ya shilingi milioni 700 na iwapo mvua za masika zitawahi kunyesha, almashauri inaweza kupata hasara kubwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Juma Kimisha, ambaye pia ni diwani wa Kata ya Nyamilangano, alisema maamuzi ya madiwani hao yatazingatiwa kwani halmashauri ilikuwa ikisubiri baraka zao katika kufanya maamuzi yake.
No comments: