LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ATAKA WANANCHI KUSHIRIKISHWA KATIKA MIRADI YA MAENDELEO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shaban Njia, Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, amewataka viongozi wa Wilaya ya Kahama mkoani humo, kuwashirikisha wananchi katika miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo ili kuongeza ari ya uwajibikaji kwa wananchi.

Telack Alisema hayo katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, kilichokaa juzi kwa lengo kujadili shughuli za maendeleo katika Halamashuri hiyo ambapo pia kihudhuriwa na Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoani Shinyanga.

"Katika shughuli za utengenezaji wa Madawati hamkuwahusisha wananchi hali iliyopelekea shughuli hiyo kufanywa na serikali tu na hivyo kugharimu fedha nyingi ambapo kama wananchi wangehusishwa wangesaidia kupunguza gharama hizo”.Alisema Telack.

Kuhusu madawati, Telack alisema yamekamilika na kwamba nguvu kubwa inaelekezwa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za walimu.

No comments:

Powered by Blogger.