LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA MKOANI MWANZA AWATAHADHARISHA WAKAZI WA WILAYA HIYO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe.Mary Tesha, akizungumza juzi jumamosi katika Uzinduzi wa Mpango wa Ugawaji wa Vyandarua kupitia Kliniki ya wajawazito na Mtoto mkoani Mwanza, uliofanyika katika Uwanja wa MTC-Kona ya Nyegezi Jijini Mwanza.
Na Vesterjtz, Mwanza
Mratibu wa malaria Mkoa wa Mwanza Dk Saula Baichumila akizungumza juzi jumamosi katika Uzinduzi wa Mpango wa Ugawaji wa Vyandarua kupitia Kliniki ya wajawazito na Mtoto mkoani Mwanza, uliofanyika katika Uwanja wa MTC-Kona ya Nyegezi Jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana akipima kipimo cha Malaria
Mwimbaji Khadija Kopa (wa pili kulia) akitumbuiza katika Uzinduzi wa Mpango wa Ugawaji wa Vyandarua kupitia Kliniki ya wajawazito na Mtoto mkoani Mwanza, uliofanyika katika Uwanja wa MTC-Kona ya Nyegezi Jijini Mwanza.
Msanii Izzo Buzness akitumbuiza katika Uzinduzi wa Mpango wa Ugawaji wa Vyandarua kupitia Kliniki ya wajawazito na Mtoto mkoani Mwanza, uliofanyika katika Uwanja wa MTC-Kona ya Nyegezi Jijini Mwanza.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Marry Tesha, amewataka wakazi wa Wilaya hiyo kutumia vyandarua vinavyogawiwa bure na serikali kwa mama wajawazito ili kujikingana maambukizi ya ugonjwa wa malaria.

Akizungumza jumamosi iliyopita katika uzinduzi wa mpango wa Ugawaji wa Vyandarua kupitia Kliniki ya wajawazito na Mtoto kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, mkuu huyo wa wilaya alisema wananchi wanapaswa kuachana na mila potofu kwamba vyandarua hivyo havifai.

Alisema wapo baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakivitumia vyandarua hivyo kwa matumizi ya kufugia kuku na kuvulia samaki jambo ambalo sio sahihi ambapo alionya matumizi ya namna hiyo.

“Lengo la serikali ni kuhakikisha kwamba malaria inakwisha kabisa katika nchi yetu na inatumia gharama nyingi kuleta vyandarua hivi kwenu wanachi ili muweze kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu,”alisema Tesha.

Alisema kumekuwa na imani potofu kuwa vyandarua hivyo vinavyogawiwa bure kwa wamama wajawazito vina madhara kwao jambo ambalo alisema siyo kweli kwa kuwa dawa iliyomo imehakikiwa kutokuwa na madhara kwa binadamu.

Awali akitoa taarifa wakati wa utambulisho wa mpango na ugawaji wa vyandarua hivyo kupitia kliniki ya wajawazito na watoto, mratibu wa malaria mkoani Mwanza, Dkt.Saula Baichumila, alisema wagonjwa 235 wa malaria wamepoteza maisha katika mkoa huo kwa kipindi cha miezi sita tangu mwezi januari hadi juni mwaka huu, ambapo vifo 121 ni vya watoto chini ya miaka mitano.

Alisema mkoa umeendelea kupambana na ugonjwa huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na hivyo kumekuwepo na matokeo mazuri ya ugonjwa huo kupungua.

Hata hivyo  mpango wa ugawaji wa vyandarua unaojulikana kama CHANDARUA KLINIKI ulianzishwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Misaada ya Kimataifa (USAID) ambapo jumla ya vyandarua 142,360 tayari vimesambazwa kupitia vituo mbalimbali vya Afya mkoani Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.