LIVE STREAM ADS

Header Ads

OZONA MISS LAKE ZONE 2016 ANYANG'ANYWA ZAWADI YA GARI HADHARANI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Shindano la Ozona Miss Lake Zone 2016 limeingia dosari baada ya mshindi wa shindano hilo, Eluminatha Dominick, kunyang'anywa zawadi ya gari aliyopewa.

Si taarifa nzuri maana awali waandaaji wa shindano hilo walisema zawadi ya gari hilo (Toyota Passo) ilinunuliwa kwa shilingi milioni 12 huku habari za uhakika zikidai kwamba gari hilo lilinunuliwa kwa shilingi Milioni tisa.

Gari hilo limekamatwa wakati likitoka uwanja wa ndege wa Jijini Mwanza kumsindikiza miss huo aliyekuwa akielekea Jijini Dar es salaam kwenye kambi ya mashindano ya Miss Tanzania 2016.

Hii si habari nzuri na ni zaidi ya aibu kwa Miss, lakini pia si habari njema kwa waandaaji ambao ni Flora Talents Promotion na mdhamini mkuu, kampuni ya vipodozi ya Ozona.
Tazama HAPA Ilivyokuwa.

No comments:

Powered by Blogger.