LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI YATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU MAPENDEKEZO YA BARAZA LA KIMATAIFA LA HAKI ZA BINADAMU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Serikali imesema haitakubaliana na  mapendekekezo yaliyotolewa na baraza la kimataifa la haki za binadamu ambayo yanaenda kinyume na katiba ya nchi hususani suala la mapenzi ya jinsia moja

Hayo yalibainishwa wiki hii Jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju, katika warsha ya kujadili mapendekezo yaliyotolewa na baraza hilo.

Alisema katika mapendekezo 227 yaliyotolewa, serikali iliyakubali mapendekezo 130 na kukataa 72 huku 25 yakipaswa kujadiliwa zaidi.

Alisema serikali inatambua kuwa wako baadhi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ila katiba ya nchi inapingana na vitendo hivyo vinavyoweza kuyaharibu maadili ya taifa huku akivitaka vyombo vya habari kusimama kidete kwa kuandika habari zinazopinga mapenzi ya jinsia moja.

Mratibu wa kitaifa wa mtandao wa utetezi wa haki za binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa, aliitaka serikali kutoa uhuru wa kupatikana kwa habari bila kuwawekea vikwazo wanahabari katika kuripoti masuala mbali mbali ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa kupata habari duniani.

No comments:

Powered by Blogger.