LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKIMBIZA MWENYE KITAIFA AWAONYA WAZAZI NA WALEZI MKOANI SHINYANGA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Tangazo muhimu

Na Shaban Njia, BMG Kahama
Mkimbiza mwenge kitaifa, Makame Nahodha Makame, amewataka wazazi na walezi katika Halmashauri ya Ushetu iliyopo Wilaya Kahama Mkoani Shinyanga kuhakikisha watoto wao wanapata fursa ya elimu ili baadaye wasiwe Vijana tegemezi tegemezi katika jamii.

Akizungumza jana na wanakijiji wa Kijiji cha Busenda, Kata ya Chona wialayni humo, Makame alisema wazazi wamekuwa na tabia ya kutowapeleka watoto shule na badala yake kuwapeleka katika shughuli za kilimo ikiwa ni pamoja na kuchunga mifugo na kuwaozesha watoto wa kike wakiwa na umri mdogo, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Alionya kwamba elimu pekee ndiyo msingi wa maisha kwa kizazi  cha sasa na kijacho na kwamba kama wazazi wataendelea na dhana ya kutowapeleka watoto wao shuleni, itafanya halmashauri ya Ushetu kuwa na asilimia kubwa ya wakazi tegemezi.

No comments:

Powered by Blogger.